Kununua $ usd

Mahsen Nyota

Member
Joined
Jul 28, 2015
Posts
17
Reaction score
12
Habari wanajamii forum nahitaji msaada wa maelezo namna ya kuweza kununua USD Money (Dola)
Mimi nafanya Biashara zangu ndogo ndogo Online, sasa mara nyingi hua nanunua DOLA na kuituma kwa ajili ya kununua mzigo, jana nilikwenda Bank mbili hivi kwa ajili ya kununua Dola lakini kila nilipoingia walikuwa wanahitaji Document yani vithibitisho kuwa ile pesa unaenda kuifanyia nini......!

MSAADA KWENU...!
KUTOKANA NA BIASHARA YANGU NILIOIRODHESHA HAPO JUU NIFANYE NINI ILI NIWEZE KUPATA HIYO HUDUMA???
 
Kwani si benki ya posta ndo wanafanya hiyo kazi? Nenda tu huko au tafuta documents tu ili mambo yasiwe mengi.

Barafu la moto
 
Soon ukikutwa na dola ni jela kwa uhujumi uchumi.

Tanzania yetu [emoji24][emoji24]
 
unafanya bishara gani??
 
Mimi nafanya Biashara zangu ndogo ndogo Online, sasa mara nyingi hua nanunua DOLA na kuituma kwa ajili ya kununua mzigo,
Je unatuma kwa njia gani?

Jibu la hili swali litanipa ufumbuzi jinsi ya kukusaidia.
 
Kama uko dar au Arusha nenda Kenya border unachenji na kuituma kununua mzigo au tafuta upande wowote wa border kati ya Tanzania nenda kanunue dollars na hukohuko Fanya kununua mzigo kisha njoo Tz kupokea


SWISSME
 
Hakuna sasa hv kuchange pesa ni Bank na lazima uwe na maelezo ya kutosheleza waenda kuzifanyia nini!?
Mbona matangazo yao yanatuchanganya sasa,kwenye matangazo wanasema ni rahisi kubadilissha hakuna kigezo chochote kile cha kubadilisha ama kununua,hebu jaribu Nmb nakumbuka wao wanachotaka ni kuwa na id mfano ya ya Taifa,ama cha mpiga kura
 
Naomba unieleweshe kidogo ukiisha zinunua unazitumaje? Mm nilikuwa najua si lazima ununue USd kwenye biashara ya mtandaoni.
 
Je unatuma kwa njia gani?

Jibu la hili swali litanipa ufumbuzi jinsi ya kukusaidia.

Mimi hua Natuma pesa kwa Agent wangu halaf yeye ndiye anatuma kwa Bank Acount ya kampuni ninayotaka kununua mzigo kwake, sasa pale ninapoenda kutuma hawataki TSH kwa vile natuma kwa Dola bas wanataka Dola tu
 
pole mno mtoa hoja,huu ni mwaka 2019 bado tunahangaika na vitu vidogo kama hivi,mtoa hoja umejiajiri mwenyewe na ni haki yako kutoka serikali yako kukurahisishia mazingira ya ujasiri mali wako,ndio maana hadi leo tunaipigia magoti serikali yetu baada ya kutengeneza mazingira ya kuifanya ndie mwajiri mkuu na hii ni wrong,kujiajiri ndio njia mwafaka;huwa nashangaa sana kunapotelewa tangazo la kazi(ualimu,afya n.k)tunahangaika kama ndio tumefunguliwa na kuuona mwanga.u must fight for this na kulalamika hakutatoa majibu ,na njia za mkato sio nzuri ni vema ukawa raia mwema wewe na familia yako.good luck
 
Tafuta bureau de change yoyote ubadilishe hela zako mkuu. unatakiwa kuwa na kitambulisho chochote.

Leo nilienda bureau de change moja kubadilisha dollar kadhaa bahati mbaya sikuwa na kitambulisho ila nilikua na bima ya afya, wakaitumia hiyo hiyo

pia kama ni vigumu kupata bureau de change, basi nenda benki ya CRDB au NBC naona wanafanya hayo mambo.

Hongera kwa biashara za kimataifa

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Asante sana Mkuu..!
 
Kama uko dar au Arusha nenda Kenya border unachenji na kuituma kununua mzigo au tafuta upande wowote wa border kati ya Tanzania nenda kanunue dollars na hukohuko Fanya kununua mzigo kisha njoo Tz kupokea


SWISSME

Nipo Dar Mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…