Katika mambo ya kipuuzi kufanywa na serikali ni hili, hivi kweli tumefikia huko? na anayetaka kwenda kutembea mfano Dubai tu nayo aende na nini? na waambia hii kitu itaathiri biashara za watu korosho cha mtoto. Itafanya Tanzania kuwa nchi ngumu kufanya biashara na kuhakikishia hutaona Mcongom, sijui mzambia kuja kariakoo tena na biashara zitakufa taratibu tunaona. Maana haiwezekani mtu aje na dola zake anataka kuchange unamwambia nenda Bank wakati rate zao mbovu halafu lete hichi sijui lete kile. Nenda Dubai maduka kubadilisha pesa kila sehemu ila lazima watakuomba ID card na utapewa risiti hicho ndio tulitakiwa kufanya, wacha wafanye biashara ila kwa utaribu wa kutoa ID card na risiti lazima watoe basi lakini sio kufunga maduka. tunajipiga risasi wenyewe, biashara imekuwa nguvu tumerudi enzi za 1980's watu wanarahisisha sisi kinyume. nani wa kuja kwetu hakuna ...