Kununua used car show room

Kununua used car show room

T.K

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2010
Posts
345
Reaction score
75
Wadau naomba kufahamishwa hasara/faida za kununua used car show room ukilinganisha na kuagiza toka Japan. Mfano kwa spacio new model cc 1500.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inategemea na Show room, kuna nyingine wana tabia ya kuuza vipuli vya magari yaliyo show room kisha kurudishia vibovu......hilo ni moja tu, kwakuwa umeuliza faida/hasara, ngoja wengine pia waseme....
 
Hilo la kubadilisha vipuli nimewahi lisikia. Je naweza jua ni show room zipi ni waaminifu kwa miji ya Arusha na Dar?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Faida ya kuagiza ni unaokoa pesa isiyopungua milion mbili mpaka tatu..hasara ya kwenda showroom ni kupata asara ya milion mbili mpaka tatu hivi maana na wao wanatafuta faida,lakini pia unaweza uziwa gari imetumika huko Japan na hapa hapa nchini kisha ikapigwa rangi na service ya nguvu japo unakuta ilishapiga Dar to Kasulu kama mala mia tisa hivi.

JAH RASTAFARI MORNING AFRICA
 
Kama umejipanga, fanya kuagiza tu ndugu, unaweza negotiate bei kwenye kuagiza na ikakusaidia kwenye kulipa kodi hapa bongo, mara nyingine ni bora kuvizia gari za mnada za TRA pale bandarini, walioshindwa kuzitoa wanaziacha, wee unaenda kuokota kwa bei nzuri ila ndo upate mtu wa kukuchezeshea, uandae na 500k ya kumtoa.
 
Wadau naomba kufahamishwa hasara/faida za kununua used car show room ukilinganisha na kuagiza toka Japan. Mfano kwa spacio new model cc 1500.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sijawahi kuwaza kununua gari show room. Ukinunua gari kwa kuagiza moja kwa moja toka Japan una possibility ya kupata gari iliyo katika hali nzuri zaidi kuliko kununua show room. Ushauri wangu kwako.... agiza gari unayoipenda toka Japan... Vumilia baada ya wiki 4-6 gari yako IPO bandarini..... Saaafi.
 
Faida ya kuagiza ni unaokoa pesa isiyopungua milion mbili mpaka tatu..hasara ya kwenda showroom ni kupata asara ya milion mbili mpaka tatu hivi maana na wao wanatafuta faida,lakini pia unaweza uziwa gari imetumika huko Japan na hapa hapa nchini kisha ikapigwa rangi na service ya nguvu japo unakuta ilishapiga Dar to Kasulu kama mala mia tisa hivi.

JAH RASTAFARI MORNING AFRICA
Asante kwa mchango wako. Ukisema uagize unachukua muda gani kutoka kuagiza hadi gari kuwa cleared bandarini assume kuwa hela ya kulipia gharama zote ipo
 
Inategemea na Show room, kuna nyingine wana tabia ya kuuza vipuli vya magari yaliyo show room kisha kurudishia vibovu......hilo ni moja tu, kwakuwa umeuliza faida/hasara, ngoja wengine pia waseme....
Hasara ni: hua wana mchezo wa kushusha mileage.

Hio ndio shida yao nyingine kubwa, na gari nyingi wanazipiga rangi.
 
Asante kwa mchango wako. Ukisema uagize unachukua muda gani kutoka kuagiza hadi gari kuwa cleared bandarini assume kuwa hela ya kulipia gharama zote ipo
Wiki nne unakua na chuma mkononi

JAH RASTAFARI MORNING AFRICA
 
Wakuu nijuzeni bei ya show room na ya japan direct ipi kubwa??
Kubwa huwa ni ya show room. Sababu wa show room ataongeza gharama kwa ajili ya kupata faida. Wote mnaweza ingiza gari X kwa milioni 9 jumla, show room inaongezwa 2.5mil hadi 3mil.
 
Huu uzi umenisaidia sana! Wiki hii nilikuwa na safari ya kwenda showroom wamenikosa.
 
JF idumu!
Hata mimi mkuu nilishaweka mawazo ya kwenda show room. Ila kwa michango ya wadau humu ni bora kuvuta subira kuagiza tu kama nitalazimika kusubiri wiki nne. Maana wanasema haraka haraka haina baraka na subira yavuta heri.
 
Kubwa huwa ni ya show room. Sababu wa show room ataongeza gharama kwa ajili ya kupata faida. Wote mnaweza ingiza gari X kwa milioni 9 jumla, show room inaongezwa 2.5mil hadi 3mil.
Anhaa kumbe mkuu

Sent from my iPhone 5s using Tapatalk
 
Nyie ndio mnaofanya shilingi izidi kuadimika,
Akinunua show room mzunguko wa pesa unakuwa kidogo.
 
Comparison ya bei tafadhali mkuu

Sent from my iPhone 5s using Tapatalk
Gari ambayo utainunua Japan mpaka unaimiliki inaweza ikawa 11M na gari hiyohiyo unaweza kuinunua hapa bongo kwa 15M.
 
Back
Top Bottom