Kunusuru sok letu, huu ni ushauri wangu.

Kunusuru sok letu, huu ni ushauri wangu.

TAWA

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2013
Posts
3,674
Reaction score
1,572
"Tanzania ni kichwa cha mwehu". Ndivyo tunavyotafsirika katika medani ya mpira wa miguu. Sibezi jitihada zinazofanywa na TFF kunusuru hali hiyo ya soka nchini. Lakini yote hayo ni sawa na kupigana na adui usiyemjua. Hakika TFF hawafahamu adui mkuu wa soka hapa nchini. Haya ni matatizo machache ya soka Tanzania.
- Ujuzi katika utawala wa soka la Tanzania. Viongozi wengi wanaochaguliwa kuongoza soka la Tanzania "siyo mazalia ya mpira" kwani wengi huongoza soka kwa utashi wao na mihemko ya vijiweni.
- ubadhilifu na rushwa. Hili ni tatizo lingine katika soka letu. Kila kukicha mfumo wa uuzaji wa tiketi za kuingia viwanjani unabadilika. Lakini pia rushwa inachangia hata upangaji wa matokeo kwa baadhi ya mechi.
- ubovu wa baadhi ya waamuzi wanaochezesha ligi za madarja tofauti hasa ligi daraja la kwanza na ligi kuu.
- hakuna mipango endelevu ya soka hapa nchini. Uwezi ukaunda timu ya taifa eti "maboresho" kwa kutumia mabonanza huku ukiacha michezo kama vile umiseta na umitashunta ikiendelea huku hakuna hata mwakilishi yeyote toka TFF.
NINI KIFANYIKE:
1. Tuajiri mkurugenzi wa ufundi ambaye ni expert katika soka toka katika nchi zilizoendelea kisoka kama vile Argentina, Brazil, France, England etc ambaye atakuwa walau "mkurugenzi wa soka kweli". Mfano huwezi kumuajiri kocha kama Hans Van Pruign kuwa kocha wa timu ya taifa huku atawajibika kwa mkurugenzi wa soka ambaye haeleweki. Tukiwa na mkurugenzi bora wa soka hata julio anafaa kuwa kocha wa timu ya taifa.
2. Tuwe na mipango endelevu itakayotuvusha, siyo tuimbe tu kwamba tutacheza CAN 2017 huku hakuna mipango yoyote. Mfano vijana wanaolelewa na TSN waaminiwe na watengewe fadha za kutosha kuwaendeleza. Pia TFF izisaidie academy za soka changa ili kuzalisha wachezaji bora wenye misingi ya soka.
3. Kila mtu TFF afanye kazi yake kwa namna inavyotakiwa. Mkurugenzi wa ufundi anakaaje ofisini kama bosi!? Mkurugenzi wa ufundi azurure kutafuta vipaji. Vipaji vingi vipo mikoani, mpira hauchezwi Dar es salaam tu hapo karume.
4. Ligi iboreshwe kwa kuongezewa timu walau zifike 18 ili kuleta ushindani wa kweli na kupata bingwa anayestahili. Mfano, timu ya Tanzania prison katika msimu wa 2014/2015 imeshinda mechi tano tu lakini bado ipo ligi kuu. Pia zawadi kwa bingwa iboreshwe iendane na hadhi ya ligi.
Miundo mbinu ya soka iboreshwe kama vile viwanja nk.
Tukiyafanya hayo uenda tukafanikiwa.
Tukosoane kwa staha.
 
Back
Top Bottom