Kunusuru uharibifu miundombinu ya umma; Serikali isitishe biashara ya chuma chakavu

Kunusuru uharibifu miundombinu ya umma; Serikali isitishe biashara ya chuma chakavu

Stuxnet

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2011
Posts
13,417
Reaction score
23,310
Screenshot_20241112_084831_Chrome.jpg
Screenshot_20241112_085458_Chrome.jpg

BIASHARA ya vyuma chakavu imeenea karibu kila kona ya nchi, watu wanajitafutia riziki kwa kutafuta vyuma hivyo, kuvikusanya na kwenda kuviuza ili wajipatie fedha kwa ajili ya matumizi yao ya kila siku.

Hata hivyo, ninadhani biashara hiyo inapaswa kumulikwa, kwani baadhi ya watu wanaokusanya vyuma hivyo chakavu, wanaharibu na kuiba miundombinu mbalimbali ikiwamo ya barabara.

Kwa mfano, unaweza kukuta pembeni mwa kingo za madaraja kumefungwa vyuma, lakini baadhi ya watu wamekuwa wakituhumiwa kujihusisha kuvifungua na kwenda kuviuza kama chuma chakavu.

Wakati vyuma hivyo viking'olewa, wengine wanachukua mifuniko ya chemba za maji ya mvua na kwenda kuiuza kama chuma chakavu, kitendo ambacho ni wazi kuwa ni hujuma.

Biashara ya ukusanyaji, usafirishaji, uhifadhi na urejelezaji wa chuma chakavu si mbaya, kwani kwa namna moja au nyingine unasaidia kutunza mazingira, lakini inapofikia kuharibu miundombinu, ninadhani unageuka kuwa hujuma, hivyo wenye mchezo huo wangemulikwa.

Ni vyema wanaofanya biashara ya chuma chakavu wasiwe chanzo cha uharibifu wa miundombinu ya barabara na maeneo mengine, kwani uharibifu huo sasa umesababisha kusiwapo mifuniko ya chuma kwenye chemba za maji ya mvua katika baadhi ya maeneo.

Limekuwa jambo la kawaida kukuta mfuniko umeondolewa na badala yake limewekwa gurudumu au matawi ya miti kama ishara ya kuwatambulisha madereva kuwa kuna shimo mbele.

Hujuma za aina hiyo, ninadhani ndizo zimesababisha hata mkandarasi anayepanua Barabara ya Morogoro kuanzia Kimara hadi Ubungo, Dar es Salaam kuamua kuweka mifuniko ya zege kwenye chemba mpya.

Ninadhani ni wakati sasa wafanyabiashara wa chuma chakavu kuwa waaminifu na kuepuka kujihusisha kuhujumu miundombinu. Wafanye kazi na serikali kwa kuwafichua wanaoharibu miundombinu na kuiuza kama chuma chakavu, kwani kitendo hicho ni sawa na uhujumu uchumi.

Binafsi ninaamini kwamba mtu akifanya biashara yake kwa kufuata taratibu, hawezi kujihusisha na hujuma. Hivyo, hata wanaokusanya chuma chakavu kutoka kwa watu mbalimbali, wangekuwa makini.

Katika maisha ya sasa, kuna baadhi ya watu wapo tayari kufanya hujuma ili wajipatie fedha, wafanyabiashara wanatakiwa kuwa makini na watu wa aina hiyo ili wasiwaingize katika mtego.

Biashara hiyo imeongeza ajira kwa baadhi ya vijana wanaopita mitaani na kuokota vyuma hivyo, lakini inawezekana wapo baadhi ambao wanajihusisha na wizi wa miundombinu na kuiuza kama chuma chakavu.

Kwa hiyo, wafanyabiashara wa chuma chakavu wangejihadhari na ununuzi wa vyuma vinatokana na miundombinu ya serikali, kwani wanaowapa vyuma hivyo wapo tayari kufanya hujuma wapate fedha.

Yapo baadhi ya maeneo, wameiba hadi vibati vya anuani za makazi na kwenda kuiuza kama chuma chakavu. Yote hayo ni hujuma na kuharibu kodi za wananchi zilizotumika kutengeneza vibati hivyo.

Inasikitisha kuona ujenzi wa barabara umekamilika na miundombinu yake, lakini baada ya muda mfupi, mifuniko ya chemba za maji ya mvua haipo au vyuma vya kingo za barabara vimeng'olewa.

Huo sio uzalendo. Kama tunashindwa kulinda miundombinu yetu tunataka aje nani atulindie? Hapa kuna tatizo la ukosefu wa uzalendo kwa kushindwa kulinda na kuthamini vitu vyetu.

Tutafakari kisha tuchukue hatua, kwani hakuna mtu kutoka nje atakayekuja kulindia miundombinu bali ni sisi Watanzania wenyewe, ingawa wengine huwa wanasema hiyo ni mali ya umma au haina mwenyewe.

Mawazo hayo ndio yanayosababisha hata tunapoona hujuma zinafanyika, hatuchukui hatua zozote za kuhakikisha tunazuia, badala tunaona ni jambo la kawaida kukuta mifuniko ya chemba katika barabara imeibiwa huku kukiwa kumefunikwa na gurudumu au majani.

Ushauri:
Serikali isitishe biashara ya chuma chakavu mara moja.
 
Hela ya chuma ni tamu jamani.

Ukikamatwa na nyara za serikali ni kufilisiwa ka mtaji kako, iko wazi.
 
Kwa hiyo mwisho wa siku hivi vyuma chakavu viende wapi

Cha msingi serikali ilinde miundombinu yake ,basi

Maana si kila chuma chakavu kimetoka kwenye hiyo miundo mbinu
Kwani zamani vyuma chakavu vikikwenda wapi? Maana enzi za Ali Hassan Mwinyi na JKN hakukuwa biashara hii
 
Hayo ni mawazo ya kimaskini sanaa
Tanzania ìko nyuma kimaendeleo kutokana na mawazo kama ya kwako HUMAN ERROR !! Yaani badala ya kusema nini kifanyike unaishiaa kusema eti mawazo ya kimaskini.

Nyinyi ndiyo wahujumu wenyewe wa miundombinu
 
Ninavyojua wanaonunua vyuma chakavu hawanunui hata siku moja mali ya serikal, kama kingo za barabar, nyaya za umeme,reli n.k na wanavijua kabisa na wanajua msala wake na hata huko kwa wahindi wanapopeleka vinachambuliwa, ni mim muokota vyuma mzoef 15 yrs
 
Ninavyojua wanaonunua vyuma chakavu hawanunui hata siku moja mali ya serikal, kama kingo za barabar, nyaya za umeme,reli n.k na wanavijua kabisa na wanajua msala wake na hata huko kwa wahindi wanapopeleka vinachambuliwa, ni mim muokota vyuma mzoef 15 yrs
Exactly, hakuna mnunuzi wa chuma chakavu atanunua chuma cha reli, akikuona macho atakufukuza kama jambazi
 
Exactly, hakuna mnunuzi wa chuma chakavu atanunua chuma cha reli, akikuona macho atakufukuza kama jambazi
tanesco wakipitisha nyaya zao za umeme na machuma wanaweza wakaziacha hapo chini hata mwezi nyaya na vyuma na hakuna mlinzi na ni porin lakin hamna anaegusa hadi wanakuja kumalizia kazi yao, wanajua hamna atakaegusa maana huna pakuvipeleka
 
Ninavyojua wanaonunua vyuma chakavu hawanunui hata siku moja mali ya serikal, kama kingo za barabar, nyaya za umeme,reli n.k na wanavijua kabisa na wanajua msala wake na hata huko kwa wahindi wanapopeleka vinachambuliwa, ni mim muokota vyuma mzoef 15 yrs
Je hao walioshikwa na copper za SGR wenyewe wanapeleka wapi?
 
Binafsi siwezi kua mzalendo, kama kuna fursa ya kuchoa hayo madude na pesa ipo nayachomoa tu.
 
sio hoja ngeni. wadau washatoa sana rai serikali kiziwi haina mpango
Kwenye hili la SGR lazima action ichukuliwe. Napendekeza mengine kama ifuatavyo:-
Options hizi hapa:-
1.Waweke fensi ya volt 400
2.Polisi wafanye kazi kama Operation MKIRU
3.Ban biashara ya chuma chakavu
4. Deploy ghost informers ktk vijiji vyote reli inakopita japo kwa gharama kidogo. Pia ni kutengeneza ajira kwa wananchi.
Watapata taarifa za kialifu kabla ya uhalifu kutendeka
 
Yanaweza yakawa mawazo ya kimaskini lakini yakawa na tija. Kwani wewe unaweza kufanyaje kukomesha uharibufu wa miundombinu.


Anyway wewe ni mfanyabiashara wa chma chakavu pale Buguruni, ngoja nikuache
Japo serikali haifanyi biashara, inaweza kuwa na kampuni au shirika lake ambalo ndio pekee lipewe haki ya kufanya biashara ya chuma chakavu (kuuza na kununua).
Yaani anayehitaji chuma chakavu lazima anunue kutoka kwenye hiyo kampuni ya serikali tu, vinginevyo anachukuliwa kuwa ni mwizi tu.
Hii ndio itapunguza uhujumu wa miundombinu. Hata wauzaji wadogo wakiuzia serikali, lazima serikali ijiridhishe kuwa vyuma hivyo vimetoka sehemu salama.
 
Back
Top Bottom