Kunyimwa goli: Yanga yaenda CAF kudai point 3

Utopolo umeenza kujizihilisha huko kimataifa
 
Kazi imeanza. Huko kwenye hizo ofisi ikiwezekana kuwe na ofisi maalum chumba kikubwa cha barua za malalamiko. Wawasiliane na TFF kwa maelekezo kuwa ni mafaili gani yanahimili karatasi nyingi maana wana uzoefu.
Kwa mtazamo wangu walichofanya Yanga ni cha maana zaidi kwa timu zote zinazoshiriki. Kwa sababu wasipotoa taarifa juu ya haya maamuzi mabovu ya Marefa, leo itatokea kwa Yanga lakini kesho itakuwa kwa Simba au timu nyingine yoyote ile. Hiyo ndio maana halisi ya uongozi badala ya kulalamika tu kwenye mitandao. Natumaini CAF watalifanyia kazi suala hilo ili lisijitokeze kwenye michezo ijayo.
 
Mwandishi wa hiyo barua kuna mahala kataja kudai point tatu?? Au hayo ni maoni yako?? AU unadhani kila anayelalamika anataka point tatu? No wonder nyie ni Mbumbumbu FC
 
Simba na Yanga zisha watoa akili watu, kila kitu ni kupingana tu ingekua timu ya nje wangesifia
 
Ukitaka kupata kitu jadili na Wenye uelewa kama wewe. Mimi kwako nimepata kitu. Kuandika barua ya malalamiko kuhusu Jambo ambalo timu haikuridhika ni haki yao. Umetoa mifano mizuri na si hiyo tu. Japo matokeo yatabaki kama yalivyo lakini angalau imeonekana kuna kitu hakikuwa Sawa. Watanzania wamezoea utawala unaowakandamiza bila kujitetea, wanapoona Mtu anaanza kudai haki iliyopindishwa wanaona ni ajabu. Rivers na USM waliandika kulalamikia Mambo ya nje na ndani ya uwanja. Lakini Simba pia waliwahi kuandika barua kulalamika dhidi ya maamuzi mabovu yaliyoipa Kaiser chiefs goli la offside. Lalamikeni mnapoona kuna kitu hakikwenda Sawa, ni haki yenu.
 
AZAM nao wangepeleka malalamishi yao TFF kwa ile dhulma mliyowafanyia kupitia lomalisa na penalty zenu za mchongo mlizokuwa mnapewa kwenye NBC premier league.
 
AZAM nao wangepeleka malalamishi yao TFF kwa ile dhulma mliyowafanyia kupitia lomalisa na penalty zenu za mchongo mlizokuwa mnapewa kwenye NBC premier league.
Wana haki ya kulalamika kuna ubaya gani kama sheria ina wapa nafasi ya kulalamika? au ndio CCM isha tufundisha kukaa kimya
 
Humu kuna watu unaweza ku question uwezo wao wa kufikiria unakuta ni platinum member ila vitu anavyo ongea unajiuliza hii ndio JF ya great thinkers au ni nyingine! USMA walifanyiwa fujo wakalamika CAF shangwe zikaibuka humu humu leo watu wale wale wamegeuka
 
Huwa sina Shaka na OKWI maana siku moja aliwahi kunishauri nisimchukulie serious Kwa Kila Jambo, inawezekana hata hili hayuko serious.
 
Pamoja na uamuzi wa refa kuwa ndiyo wa mwisho, bado huwaga wanapewa adhabu..!! Au hujui hilo?
Wewe ndiye hujui nimemaanisha nini. Refa anaweza kuchukuliwa hatua lakini maamuzi yaliyotolewa uwanjani hayawezi kubadilishwa. Umekurupuka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…