Kunyimwa goli: Yanga yaenda CAF kudai point 3

Baada ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Medeama, uongozi wa klabu ya Yanga umeliandikia barua Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) KULALAMIKA uamuzi mbaya ulioonyeshwa na mwamuzi aliyechezesha mchezo wao huo
.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Rodgers Gumbo alikiri kuandika barua ya MALALAMIKO kwa CAF “Ni kweli tumepeleka barua ya malalamiko kwa CAF kutokana na kuwa na ushahidi wa matukio ambayo ni wazi hatukutendewa haki ambayo ni pamoja na rafu ambayo mchezaji wetu Nickson Kibabage alichezewa na mchezaji wa Medeama ambaye alistahili kuonyeshwa kadi nyekundu lakini refa hakufanya hivyo.
.
“Lakini pia kuna tukio la bao letu halali ambalo Kibabage alifunga lakini refa akalikataa akiwaaminisha watazamaji na wachezaji kuwa waliotea hivyo sio bao sahihi lakini baada ya kulitazama kwenye video tumebaini uonevu; Tumewaandikia ili wajue nini cha kufanya kwa sababu matukio kama yale yananyima timu haki ya kupata ushindi na kuipa nyingine matokeo ambayo haijastahili,” alisema Gumbo

My Take
Utopolo at work
Sasa hujaweka kifungu kinachodai point tatu?
 
Mwasibu wa mashoga vipi upo?
 
Afu mtu ana beji ya platinum member na uchokooh wote huu...? Kwahiyo ni ajabu yanga kuandika barua juu ya maamzi ya refa yenye viashiria vya rushwa?.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kumekuchaaa!!
Malalamiko FC, jamani huku sio losers, hakuna mchekea.
Wooooiiiiiiiiiih
 
Ni vizuri kuwaandikia barua CAF, Lakini sidhani kama kuna sheria au kanuni ambayo inaweza kuipa Yanga ushindi kwa maamuzi mabaya yaliyofanywa na muamuzi wa mchezo kwa kukataa goli halali, kilichobaki wabadilishe sheria au waanzishe matumizi ya VAR katika group stage.
Ninavyojua sheria za mpira ni kuwa uumuzi wa refarii na wasaidizi wake ndio wa mwisho hata kama ni uamuzi mbovu wa waziwazi. Sana sana ni kuwa refarii huyo na wasaidizi wake wanaweza kuchukuliwa hatua za kinidhamu lakini matokeo ya uwanjani hayabadiliki.
 
Ni vizuri kuwaandikia barua CAF, Lakini sidhani kama kuna sheria au kanuni ambayo inaweza kuipa Yanga ushindi kwa maamuzi mabaya yaliyofanywa na muamuzi wa mchezo kwa kukataa goli halali, kilichobaki wabadilishe sheria au waanzishe matumizi ya VAR katika group stage.
Nilivyoelewa imetuma malalamiko na si kuomba ushindi wa mezani au match irudiwe,
 
Tangu lini mbumbumbu ukawa na akili? nmesema matokeo yanafutwa sio kupewa points au unataka nikupe reference?

Mpira ulishaisha subirini mechi zinazofuata, hayo mengine tuwaachie waganga wa kienyeji, na kama CAF watawajibu barua yenye sababu kama hizo basi mshukuru sana, lakini hapo hakuna issue!
 
Attachments

  • GAku6meWYAAa6ib.jpeg.jpg
    GAku6meWYAAa6ib.jpeg.jpg
    58.8 KB · Views: 1
Back
Top Bottom