Ndio mfumo uliopo huo lakini una mushkeli. Wakati tupo mwaka wa pili chuoni ilitokea incident kama hiyo, watu hawakusaini pesa zao, chuo kikadai zimerudi bodi. Vijana wakaenda bodi sio kudai pesa zirudi chuo bali wakataka wapewe barua maalum zinaonyesha kuwa hawakulipiwa 2nd semester of 2nd year.
Hapo ndipo bomu lilipolipuka, kumbe zile pesa bado zilikwepo chuo, maofisa wa chuo na bodi kwa pamoja walikuwa wanasubiri jamaa wamalize waje kupiga ile pesa at the end jamaa waje kudaiwa kama walipewa. Haikupita muda, vitabu vikaletwa tena chuo na watu wakasaini kama kawaida, watu walisaini 2nd semester fee of the 2nd year wakati tuko last semester 3rd year.