KERO Kunyimwa vyeti wahitimu wa chuo cha Western Tanganyika, Kigoma

KERO Kunyimwa vyeti wahitimu wa chuo cha Western Tanganyika, Kigoma

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Dick Osewe

New Member
Joined
Apr 18, 2024
Posts
3
Reaction score
1
Naomba niwasilishe kero yangu inayonisumbua nikiwa pamoja na wenzangu tupate ufumbuzi.

Tunaomba kujua ni lini chuo cha Western Tanganyika kilichopo kigoma itawapa wanafunzi wake waliohitimu chuo September 2022 kozi ya pharmacy ngazi ya cheti maana waliwaambia wakae vyeti vitatoka na hadi kufikia April 01 NACTEVET ilitoa taarifa vyeti vishatoka na vipo ofisi zao, kila chuo ifatilie na iwachukulie wanafunzi wake vyeti ila mpaka sasa chuo cha Western haijatoa taarifa yoyote kuhusu vyeti vya hao wahitimu wa 2022 huku wengine washafanya hadi mtihani wa leseni na wamenyimwa leseni zao kisa kutoambatanisha vyeti vyao.

Kilichopo nyuma ya pazia chuo kinawalazimisha wanafunzi kumaliza diploma huku wengine hawana uwezo wa kuendelea na masomo wakudai hawatoi vyeti vya mwaka wa pili.

Tunaomba kujua ni lini chuo hicho kitawapa takriban wahitimu 20 vyeti vyao vya taluuma kuliko kukaa kimya huku vyeti vimetoka tangu April 01.

Naomba msaada tafadhali.
😭😭😭😭
 
Back
Top Bottom