Hivi kuna ukweli ndani yake kuwa wanaume wanaonyonya lips za wanawake waliopaka lipshine, hupelekea kupatwa na Hepatisis B?
- Tunachokijua
- Homa ya ini (Hepatitis) uvimbe unaotokea kwenye ini ambao huambatana na utengenezwaji wa makovu.
Tatizo hili linaweza kuwa la muda mfupi ikiwa litadumu kwa kipindi kisicho zidi miezi 6, lakini linaweza kuwa sugu ikiwa litaendelea kuwepo kwa zaidi ya miezi 6.
Takriban watu milioni 500 duniani ni waathirika wa ugonjwa huu.
Uambukizwaji wa Homa ya ini aina B (Hepatitis B)
Husababishwa na vimelea vya virusi wa homa ya ini aina B (HBV). Ni ugonjwa ambao mara nyingi hudumu kwa muda mrefu.
Mtu anaweza kupata ugonjwa huu kupitia shahawa, damu pamoja na mazao yake pamoja na majimaji ya mwili.
Mazingira na hali hatarishi zinazoweza kusababisha maambukizi ya ugonjwa huu ni;
- Kupokea damu ya mtu mwenye ugonjwa
- Wafanyakazi wa afya kwa kuwa hukutana na damu mara kwa mara
- Kushirikiana vitu vyenye ncha kali
- Kufanya usafishaji wa damu kupitia huduma ya figo za nje, maarufu kama dialysis
- Mama kwa mtoto wakati wa kujifungua
- Wakati wa ngono ya aina yoyote ile kutoka kwenye majimaji ya uke, au shahawa za mwanaume
- Kwenye mazingira yaliyo na udhibiti mkubwa hasa magerezani na vituo vya wagonjwa wa akili
Pia, matumizi ya lipshine kwa wanawake hayachangii maambukizi ya ugonjwa huu kwa namna yoyote ile.
Njia zingine kama kukumbatiana, chafya, kikohozi, maziwa ya mama wakati wa kunyonyesha havina pia uwezo wa kusababisha maambukizi ya ugonjwa wa homa ya ini.
Matibabu yake
Ugonjwa wa homa ya ini aina B hutibiwa kwa kutumia dawa za virusi. Mgonjwa anapaswa kutumia dawa zake kwa kufuata masharti sahihi ili kufanikisha uponaji ndani ya muda unaotazamiwa.
Jikinge na ugonjwa huu ambao ni hatari kwa afya. Huwa na uwezo mara 50-100 wa kushambulia na kuambukiza kuzidi VVU.