KWELI Kunyonyesha zaidi titi moja kuliko lingine huweza kufanya linalonyonywa kuwa kubwa kuliko lingine kwa kipindi cha unyonyeshaji

KWELI Kunyonyesha zaidi titi moja kuliko lingine huweza kufanya linalonyonywa kuwa kubwa kuliko lingine kwa kipindi cha unyonyeshaji

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
1729853737240.png
 
Tunachokijua
Kunyonyesha ni ulishaji wa watoto wachanga na wadogo kwa maziwa kutoka kwenye titi la mwanamke. Wataalamu wa afya wanapendekeza kunyonyesha kuanzia saa ya kwanza ya maisha ya mtoto na kuendelea mara nyingi na kwa kadiri mtoto anavyotaka.
1730094639973-png.3136897
Katika mchakato wa unyonyeshaji huweza kutokea Mama akawa anamnyonyesha mtoto titi moja zaidi ya lingine au kumnyonyesha titi moja tu kutokana na sababu mbalimbali kama Mama kuwa na vidonda kwenye chuchu, mtoto kupendelea titi moja kwa kuwa lina maziwa mengi kuliko lingine na sababu nyinginezo.

Katika hali hiyo ya mtoto kunyonya titi moja zaidi au moja pekee, kumekuwepo na hoja kuwa Mama anayenyonyesha titi moja zaidi au moja pekee itamsababishia kuwa na Titi moja kubwa na moja dogo, yaani linalonyonywa kuwa Kubwa zaidi ya lile lisilonyonywa au kunyonywa sana na mtoto.

Je, Ukweli ni Upi?

JamiiCheck imepitia Tafiti mbalimbali na kubaini kuwa ni hali ya kawaida titi moja kuwa na ukubwa kidogo kuliko lingine japo huwa hainokeni kirahisi.

Aidha mtoto kunyonya titi moja zaidi ya lingine mara kwa mara na kwa muda mrefu huweza kusababisha titi linalonyonywa kuwa kubwa kuliko lingine kwa sababu maziwa yatazalishwa zaidi kwenye titi linalonyonywa japo hali hiyo huwa ya muda tu kwani baada ya kuachisha kunyonyesha titi hurudi katika hali yake ya awali na kuondoa tofauti ya mlingano wa ukubwa kwa wanawake wengi ingawa baadhi ya tofauti zinaweza kubaki kwa baadhi ya wanawake.

Kwa mujibu wa Australian Breastfeeding Association Wanaeleza kuwa ni kawaida na ni jambo la kawaida, titi moja kuwa kubwa kuliko lingine iwapo mtoto atanyonyeshwa zaidi mara kwa mara titi moja kwa muda mrefu kuliko lingine kwani Titi hilo litazalisha maziwa mengi kuliko lile lisilonyonywa na hivyo kuonekana kubwa, wanaeleza kuwa hali hiyo ni ya muda tu na huisha mtoto anapoacha kunyonya, titi husinyaa na kurudi hali ya awali, aidha katika wakati wa unyonyeshaji unaweza kuvaa brazia ili kuyasawazisha.

Uzalishaji wa maziwa kwenye kila titi hutegemea na jinsi mtoto anavyonyonya. Ikiwa utanyonya zaidi kwenye upande mmoja, titi hilo litazalisha maziwa zaidi. Na ikiwa maziwa yatatolewa kidogo kwenye upande mwingine, uzalishaji wa maziwa utapungua.
Back
Top Bottom