Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 9,189
- 16,128
Habari ndugu zangu. Nimekuja kuwatisha tena. Maji ya nazi/madafu yana madini ya potasium kwa wingi sana. Matunda kama machungwa na ndizi yana potasium kwa wingi lakini hayagusi hata kidogo kwa madafu.
Sasa basi. Potasium kazi yake kubwa ndani ya mwili ni kujihusisha na masuala ya umeme. Mishipa ya fahamu, kureguralte midundo ya moyo nk nk. Madini ya potasiumu yakizidi mwilini(Hyperkalemia) husababisha moyo kupiga bila mpangilio mzuri(arrythmia) jambo hili ni hatari na linaweza sababisha kifo.
Tabu hii huwapata hasa wale wenye matatizo ya figo, maana figo inashindwa kuondoa potasium kwa kasi kama inavyoingia.
Pia sijajua namna pombe ya mnazi inatengenezwa, kama inatumia maji ya dafu basi hatari ya hyperkalemia kwa wanywa mnazi ni kubwa sana. Maana pombe mtu anaweza piga lita kadhaa. Chukua tahadhari.
=====
Taarifa hii imefanyikwa kazi kwenye Jukwaa la Jamii Check. Soma: Madafu ni hatari kwa watu wenye ugonjwa wa Figo