Kunywa maji baada ya kusikia kiu ni kujiandalia kifo cha mapema na chenye maumivu sana:

Kunywa maji baada ya kusikia kiu ni kujiandalia kifo cha mapema na chenye maumivu sana:

Mtu akiwa na M.D kwa hakika ni mtaalamu wa afya au siyo mkuu?: WaterCure | About Dr. B
Kuwa na MD tu haitoshi kumfanya mtu kuwa specialized na kujua maji kihivyo. Watu wanashaka na hizo findings eti kunywa maji baada ya kupata kiu ni hatari.
Nadhani MD aliyesoma vizuri Biochemistry na Physiology atakubaliana nami kuwa dalili ya kiu ni moja ya indicator ya kunywa maji na hiyo ni FACT hadi hapo research itakapofanywa na kuonesha kuwa kuna P value with statistically significance kuwa kunywa maji wakati una kiu ni hatari kwa afya! instead of comparing our bodies with car parts please do some research otherwise SHUT UP na usipotoshe watu!!!
 
yaani mim mwenzenu kunywa maji bila kiu nayaona mabaya lkn nikiwa na kiu ndo naweza kunywa tena hapo ndo nayaona matamuu.Tutakufa wengi.
 
yaani mim mwenzenu kunywa maji bila kiu nayaona mabaya lkn nikiwa na kiu ndo naweza kunywa tena hapo ndo nayaona matamuu.Tutakufa wengi.
anza pole pole mkuu, glasi moja huku ukiongeza moja moja kila siku, utazoea tu
 
Kuwa na MD tu haitoshi kumfanya mtu kuwa specialized na kujua maji kihivyo. Watu wanashaka na hizo findings eti kunywa maji baada ya kupata kiu ni hatari.
Nadhani MD aliyesoma vizuri Biochemistry na Physiology atakubaliana nami kuwa dalili ya kiu ni moja ya indicator ya kunywa maji na hiyo ni FACT hadi hapo research itakapofanywa na kuonesha kuwa kuna P value with statistically significance kuwa kunywa maji wakati una kiu ni hatari kwa afya! instead of comparing our bodies with car parts please do some research otherwise SHUT UP na usipotoshe watu!!!
mkuu, ma M.D waliosomea na wanaosomea Biochemistry na Physiology hawafundishwi thamani ya maji mwilini, wanafundishwa tu kuwa maji ni kitu kinachotumika kusafirishia vitu mwilini, hawafundishwi kuwa maji yanaweza kutibu BP, Kisukari, Aleji, Kansa n.k, halafu wakifundishwa haya itakuwaje?.

Lakini wanafundishwa kuwa siku utakapozidiwa umebebwa katika ambulance basi wakutundikie dripu la maji na chumvi ili kukuokoa!!! hata kama siku zingine ulipoumwa kawaida hawakukushauri unywe maji. Mhimu ni kuwa dr.Batmanghelidj alisoma udaktari mpaka ngazi ya u-M.D bila kufundishwa chochote kuwa maji ni jibu kwa magonjwa mengi yanayomkabili binadamu, aliligunduwa mwenyewe hilo akiwa gerezani akitumikia kifungo chake kama mfungwa wa kisiasa na kuamua kuacha kuwatibu wagonjwa wake kwa kutumia maji tu na si madawa. Soma zaidi historia yake hapa: WaterCure | About Dr. B

Usiwe na shaka na finding hizi, just find out yourself what is the truth do not WAIT for me to prove that 2 u

www.maajabuyamaji.com
 
Huwezi amini mkuu, tokea asubuhi 06:30am mpaka saa hizi 01:57pm, nimeshakunywa lita 2.5, mpaka zifike angalau 3. Afya yangu ni nzuri, magonjwa madogomadogo kwangu mwiko! Karibu,
 
Kuna tofauti ya NDEGE, WANYAMA na BINADAMU - ndio maana hata vyakula viko tofauti - BINADAMU WANAKULA VILIVYOPIKWA NA HAO WENGINE VIBICHI [EXCEPT MATUNDA NA BAADHI YA VEGETABLES) PIA VIUMBE WANATOFAUTIANA KATIKA ULAJI/UNYWAJI WAO - NA NDIVYO MUNGU ALIVYOWAUMBA

1. Bata ni ndege - lakini anakunywa maji kushinda Kuku ambaye pia ni ndege
2. Panya kama amefungiwa kwenye box - anaweza kuwa busy kutafuna kilichopo (hata kama hakuna maji anaishi)

KWA BINADAMU - UMUHIMU NI KUHAKIKISHA "URINE" (AU MKOJO WAKO) NI MWEUPE MARA ZOTE - UKIWA YELLOW - THEN KUNYWA MAJI YANAHITAJIKA MWILINI

Mimi sio daktari - kama una swali mwulize DAKTARI
 
Usifananishe chuma na mtu. Rate/coeficiant ya expansion zinatofautiana pia. Mbona binadamu hapati kutu japo ukimweka kwenye mazingira sawa na msumari?
 
http://maajabuyamaji.com/

KUNYWA MAJI BAADA YA KUSIKIA KIU NI KUJIANDALIA KIFO CHA MAPEMA NA CHENYE MAUMIVU SANA:

Muda gani unamwagilia maji bustani yako? Kwa hakika ni asubuhi au jioni na si saa nane mchana wakati jua tayari likisha kuwa kali – la sivyo mimea itakufa. Pia ukitembea umbali mrefu na gari na ghafla maji yakaisha katika injini haushuki tu na kuongeza mengine papo kwa papo, utasubiri injini ipowe ndipo uongeze mengine – la sivyo injini ya gari (ambayo ni chuma) itakufa.

Hivyo binadamu kuendelea kusubiri kiu au mdomo ukauke ndipo anywe maji, huwa anajiandalia kifo mwenyewe cha mapema na chenye maumivu sana. '‘Mwili wa binadamu unapopungukiwa maji hutoa ishara (indicators), tumeziita ishara hizo kuwa ni magonjwa, hauumwi, una kiu, usiitibu kiu na madawa – dr. fereydoon Batmanghelidj'’.

Hivyo magonjwa kama maumivu, pumu, aleji/mzio, shinikizo la damu, kisukari,utipwatipwa, kansa, kuzeeka mapema na mengine mengi; yote haya ni ishara tu za mwili kutuambia kuwa tunapungukiwa maji, yaani tunaumwa kiu!!.

kiu hutibika kwa maji tena bila gharama yeyote!.

Magonjwa ni moja ya maadui wetu watatu tuliotangaza kuendelea kupigana naye mpaka tumshinde mara baada ya kupata uhuru kutoka kwa wakoloni mwaka1961. Ni zaidi ya nusu karne sasa bado tungali na adui huyu anayezidi kutia hofu mamilioni ya watu.
Maajabuyamaji.com inaitaja sababu ya maradhi kuendelea kututesa kuwa ni mazoea yetu kusubiri kiu ndipo tunywe maji. Inajulikana wazi kuwa maji ni uhai. maajabuyamaji.com inafafanua sababu za maji kuitwa ni uhai, inaeleza madhara yatokeayo mwilini inapotokea tunaipa miili yetu maji ya mgawo (yaani tunapokunywa maji baada ya kusikia kiu).

Kumbe kwa kutumia maji tu yale tunayoyanywa kila siku tunaweza kujikinga na kujitibu magonjwa mengi bila idadi na hatimaye kumshinda adui maradhi na hivyo kujipunguzia gharama sisi wenyewe na serikali kwa ujumla.

Maajabuyamaji.com inafundisha pamoja na mambo mengine: kazi za maji mwilini mpaka kuitwa ni uhai, namna mpya ya kuitambua kiu, na namna ya kunywa maji ili kujikinga na kujitibu na maradhi mbalimbali.

Hakuna anayependa kuugua, awe daktari, askari, kiongozi wa serikali au wa dini, mwandishi au mtangazaji, mfanyakazi au mkulima. Tovuti yako ya maajabuyamaji.com inapenda kushirikisha vyombo vya habari na wadau wengine katika kuelimisha hili, moja ya kazi mhimu za chombo cha habari ni kuelimisha jamii kwa manufaa ya jumla ya jamii nzima, kwa sababu hii tunakitoa bure kitabu cha kieletroniki (e-book) kinachoeleza kwanini kusubiri kiu ndipo tunywe maji ni kujiandalia kifo mapema na chenye maumivu sana. Kitumieni hicho kama mwongozo (user manual) wenu.

Tuendelee kusherehekea miaka 50 ya uhuru tukiwa tayari na silaha ya kumshinda adui maradhi kwa kutumia maji tu.

http://maajabuyamaji.com/

attached: maajabu ya maji e-book,download it for free

Asante sana. Tatizo langu mimi nikinywa maji nabanwa sana mkojo mara kwa mara. imekaaje hii au ni ugonjwa. Naomba kuuliza
 
Kuwa na MD tu haitoshi kumfanya mtu kuwa specialized na kujua maji kihivyo. Watu wanashaka na hizo findings eti kunywa maji baada ya kupata kiu ni hatari.
Nadhani MD aliyesoma vizuri Biochemistry na Physiology atakubaliana nami kuwa dalili ya kiu ni moja ya indicator ya kunywa maji na hiyo ni FACT hadi hapo research itakapofanywa na kuonesha kuwa kuna P value with statistically significance kuwa kunywa maji wakati una kiu ni hatari kwa afya! instead of comparing our bodies with car parts please do some research otherwise SHUT UP na usipotoshe watu!!!
Kwanza mtoa mada hajakusudia kuwa tusinywe maji wakati tunaona kiu, ni kwamba tusisubiri kuhisi kiu ndo tukanywa maji, yaani mpk indicator ikuoneshe. Tuwe na mazoea ya kunywa maji vile inavyotakikakna, kwani wengi wetu tunakunywa maji tu bt hatujui when and how.
Kiukweli, ukinywa maji inavotakikana inasaidia sn kukinga maradhi mengi na kuuweka mwili ktk hali nzuri kiafya.
Maji ni uhai.
 
Nashukuru sana mkuu, kwa hakika umeelewa. Utangulizi | maajabu ya maji
 
Asante sana. Tatizo langu mimi nikinywa maji nabanwa sana mkojo mara kwa mara. imekaaje hii au ni ugonjwa. Naomba kuuliza

Swali zuri, kama kweli unaumwa na umeamua kutumia maji kama tiba, basi soma vizuri kurasa hii yote:
je, tiba kwa kutumia maji inafanyikaje? | maajabu ya maji .

Ili maji yaweze kukutibu na kukukinga kwa kila ugonjwa ni lazima....
Kisha kunywa maji, maji yanapaswa kubaki ndani ya mwili masaa 2 mpaka 2 na nusu ili kuupa mwili muda wa kutosha kuyatumia maji hayo vizuri.

Ikiwa inakulazimu kukojoa (peeing) chini ya muda wa masaa 2 tangu unywe maji, utalazimika:

a)Kuacha kunywa maji matupu, jaribu kunywa juisi (uliyotengeneza mwenyewe) ya chungwa, ya limau, juisi ya matunda mchanganyiko, ya zabibu au juisi nyingine yeyote isipokuwa kwa watu wanaosumbuliwa na pumu (asthma) ambao hawatakiwi kunywa juisi ya chungwa. Wakati huo huo mhimu kukumbuka kuongeza robo tatu gramu za chumvi katika kila nusu lita ya juisi yako. Pia usizidishe kiasi chako unachopaswa kunywa kwa wakati mmoja, isije kuwa sababu juisi ni tamu ukashawishika kunywa nyingi kuliko unavyopaswa.

b)Ikiwa kunywa juisi hakutasaidia kupunguza kwenda bafuni kila mara, jaribu kunywa maji huku ukila mkate. Unaweza kuongeza krimu ya siagi au jamu kwenye mkate wako (the magic bagel).

Kisha kutumia mkate siku moja au mbili unaweza kupunguza sasa kiasi cha mkate mpaka nusu yake, robo yake na mwisho juisi pekee pamoja na mlo wako.

Utapaswa kurudi taratibu tena kutoka kunywa maji juisi mpaka kunywa maji matupu tena, baada ya siku kadhaa itakupasa kujaribu aunsi 2 za maji matupu nusu saa kabla ya chakula, kesho yake aunsi 4, siku inayofuata itakuwa aunsi 6 kisha 8 na kuendelea mpaka ufikie kiasi chako unachotakiwa.

c)Ikiwa kunywa maji pamoja na kula mkate au katika juisi hakukusaidii kupunguza kwenda bafuni, Glasi ya maji (ml 250) matupu ikiongezwa na kijiko (kijiko cha chakula) kimoja cha asali au sukari halisi au walau sukari nyeupe kutakutatulia tatizo hili ukiongeza na chumvi 1/8 ya kijiko cha chai , tikisa na kisha kunywa mchanganyiko huo.

d)Hakikisha unakunywa maji kwa mjibu wa kipimo chako kulingana na uzito wako. kunywa maji mengi zaidi ya kiwango chako husababisha maji kutoka nje ya mwili mapema kabla hayajatumiwa na mwili. lakini pia unapoanza kunywa maji hivi mwanzoni unaweza ndo ukawa unalazimika kwenda bafuni kila mara lakini taratibu siku hadi siku hali hiyo itaanza kupungua na kuwa kawaida, mhimu ni kuanza taratibu na kuepuka vinywaji vyenye kaffeina au alkoholi.

e)Acha kwanza kinywaji chochote cha kutengenezwa kiwandani, acha chai ya rangi na kahawa. vinywaji hivi ni mawakala vikojoshi (diuretics), huyalazimisha maji kutoka nje ya mwili mapema kabla mwili haujayatumia. utarudi kunywa chochote ikiwa utavihitaji tena vinywaji hivyo mara utakapokuwa supa tena kiafya. Acha pia uvutaji wowote wa sigara na alkoholi.

Bilashaka umewahi kusikia msemo, "Kwa sehemu kubwa tumetokana na maji", hii ndiyo sababu zaidi ya asilimia 94 ya damu yetu ni maji, zaidi yaasilimia 85 ya ubongo wetu ni maji, huku zaidi ya asilimia 75 ya sisi ni maji.

mhimu: usinywe maji mengi kwa wakati mmoja, nimeandika FOMULA ya kuitumia kila mmoja kwa kutumia uzito wake anaweza kujua ni kiasi gani cha maji anahitaji kwa siku, pia kumbuka kutumia chumvi, siku hizi watu wengi wameaminishwa kuwa chumvi ni mbaya kitu ambacho ni uongo mkubwa, jisomee namna chumvi ilivyo na umhimu mkubwa mwilini hapa: Ukweli kuhusu chumvi na maajabu yake | maajabu ya maji
 
Usifananishe chuma na mtu. Rate/coeficiant ya expansion zinatofautiana pia. Mbona binadamu hapati kutu japo ukimweka kwenye mazingira sawa na msumari?
KAKAjambazi, KWA HAKIKA mwili na vyuma ni vitu viwili tofauti, najaribu kukuelewesha namna ilivyo ni mhimu kunywa maji bila kusubiri kiu, unaona hata katika gari hausubiri mafuta yaishe kabisa katika tank la sivyo sheli utafuata mafuta kwa miguu na kidumu, utachoka sana bila shaka
 
Back
Top Bottom