Ulevi (pombe za aina yote, mvinyo n.k) vyote huwa vina alcohol aina ya Ethanol. Japokuwa Alcohol hutumiwa kwenye madawa kama viyayushaji (solvents) vya ule mchangayiko wa chemikali unaofanya dawa. Kwa ujumla wake Alcohol ni sumu.
Alcohol aina ya Ethanol ndio inayokuwa ndani ya ulevi kwa ufahamu wangu ndio inayosababisha mtu kuwa katika hali ya kulewa. Madaktari huweza kusema kiasi cha alcohol mwilini (blood alcohol level) kwa kupima ethanol iliyo kwenye damu. Na hichi ndicho kipimo wanachotumia polisi kushtaki watu wanaokamatwa wakiendesha magari na huku wamelewa.
Ama manufaa madogo ya pombe au vileo ni:
- Kupata fedha kwa wauzaji.
- Kudhaniwa na wanywaji kuwa inatoa dhiki na fikira kwa muda.
- Kutumika kuhifadhia baadhi ya vyakula.
- Kusafisha sehemu za jeraha na kuua viini.
- Kudhaniwa na wanywaji kuwa inasisimua au kuchangamsha.
- Kutumika katika mafuta aina ya virashio na manukato.
Ulimwengu wa leo umejikubalisha kwamba kuna pombe halali na haramu. Hata hivyo, manufaa haya yanazidiwa na madhara yake mengi yaliyo dhahiri na yanayo athiri afya ya mnywaji. Ubinadamu na utu wako, jamii na akili.
Inajulikana kuwa pombe ndio mama wa maasi yote, kwani kwayo hiyo pombe tumeshuhudia mauaji, ubakaji, liwaati, uvutaji wa kokeni na bangi, uzinifu, wizi, utovu wa adabu na kadhalika. Pombe uharibu afya yako hasa ini. Pombe udumaza akili na vile vile kuzuia kufikiri. Pombe husababisha ajali za barabarani na hata kupoteza maisha ya watu.
Pombe uchochea manyanyaso ndani ya majumba. Ukiwa addict wa pombe usababisha uharibifu wa kifedha. Kukosa hayaa, heshima, ustaarabu, na kufanya matendo ya kipuuzi mara nyingi. Kutoa maneano machafu, matusi. Kugombana na watu. Kutoa harufu mbaya mdomoni. Kuharibu ndoa kwa kukosa kutimiza haki za mke/me na watoto. Kupoteza wajihi wako na kuonekana mzee kabla ya umri wako... n.k n.k n.k
"Ulevi si dawa bali ni maradhi"
"Enyi Mlioamini! Bila ya shaka ulevi, na kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli, ni uchafu katika kazi ya Shetani. Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufanikiwa".
Al-Maaidah: 90
Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wa.fi.raji, wala wala.wi.ti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi.
1 Wakorintho 6:9-10