Kunywa Sumu

Kunywa Sumu

stephot

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2012
Posts
17,216
Reaction score
26,225
Jamani mnaojua sheria naombeni msaada,nina ndugu yangu alikunywa sumu lengo lake ilikuwa kujiua,tukamuwahisha hospitali lakini kabla ya hapo tuliambiwa hospitali hatatibiwa mpaka ipatikane PF3 tulifanikiwa kuipata bahati nzuri ndugu yetu huyu katibiwa na amepona kabisa,sasa nisichokielewa wale polisi walionishughulikia kuniandikia PF3 wananipigia simu kila siku ili niende tukayamalize mambo,sasa sielewi hapa kuna procedure nyingine ya kufuata au ni mambo ya kuliana hela!
 
Inawezekana wanataka wapatiwe chochote ili wazime mambo, kwa ufahamu wangu kutaka kujiua ni kosa kisheria. Kama nimekosea wanataaluma watatuelewesha zaidi....
 
aiseeeee babayangu hao polisi wape buku mbili mbili kila mmoja unafikiriwanataka nyingi
 
Kwa kifupi huyo ndugu yako amefanya kosa kisheria linaloitwa attempted suicide..!!
 
Jamani Lyamber, Kifulambute,naombenu ushauri hapa 'nisichokielewa wale polisi walionishughulikia kuniandikia PF3 wananipigia simu kila siku ili niende tukayamalize mambo,sasa sielewi hapa kuna procedure nyingine ya kufuata au ni mambo ya kuliana hela!'
 
Last edited by a moderator:

Ni hivi kimsingi polisi walitakiwe wamfungulie mashitaka kwa kosa la attempted suicide sasa si hawajafungua kesi kwaio wanataka kutumia chance hiyo wewe ukatoe hela huko polisi ili waifute kesi ingawa kimsingi kufuta kesi sidhani kama kuna gharama yeyote ile ya kulipia umeshasoma hapo mkuu..!!
 
Nimekusoma vizuri mkuu ngoja kesho niende nikawasukilize!
 
Attempted suicide ni kesi inayofunguliwa na jamhuri. Huyu ndugu nadhani hana mamlaka kufuta kesi manake sio yeye alieifungua. Nadhani ndo maana polisi wanataka wamkamue kiduchu
ingawa kimsingi kufuta kesi sidhani kama kuna gharama yeyote ile ya kulipia umeshasoma hapo mkuu..!!
 
Attempted suicide ni kesi inayofunguliwa na jamhuri. Huyu ndugu nadhani hana mamlaka kufuta kesi manake sio yeye alieifungua. Nadhani ndo maana polisi wanataka wamkamue kiduchu
Yeah jamhuri lakini si polisi hao hao..ndo wanaopeleka mahakamani ila uko sahihi mkuu na umenkumbusha ni republic pia hao hao watakao futa..!!
 
Back
Top Bottom