Kuoa/kuoana

Kuoa/kuoana

Museven

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2011
Posts
629
Reaction score
449
hivi ni lipi sahihi hapa: mwanamme anamuoa mwanamke au wanaoana?
 
mwanaume ni singular, wanaoana ni plural.
hilo swali lako halijitoshelezi afu wacha ku compare na kingereza
 
mwanaume ni singular, wanaoana ni plural.
hilo swali lako halijitoshelezi afu wacha ku compare na kingereza

sasa ya kiingereza yanatoka wapi hapa? Mi nataka kujua usahihi ni upi: mwanamme anamuoa mwanamke au mwanamme na mwanamke wanaoana?
 
soma agano la kale hasa sehemu ya mwanzo wa ndoa kwa wanadamu
 
ukweli kuoa ni kiashiria cha umiliki na kuolewa umilikiwa na mzizi wa yote ni kutokana na jamii zinazofuata mahari ambapo inachukuliwa kwamba mwanamke ni bidhaa, hivyo basi sahihi ukipenda kutumia mzizi wa hayo maneno ni kuoana.but sahihi zaidi ni kuufunga ndoa...............hii inakwenda sanjari na maeno mume au mke wangu............yote yanaashira ya ukatili wa kijinsia
 
Kwa uelewa wangu anayeoa ni mwanamume na ndivyo linavyokubalika hata katika jamii nyingi za kiafrika, kwa mfano kijana (wa kiume) wa mzee flani kamuoa binti wa mzee flani na wala si kinyume chake
 
Neno kuoa ni kupatana/kuelewana/kulandana/kufungamana. Kwa hiyo kwa mwanaume kusema KAOA ni heshima tu kwa vile mwanamke anahamia kwa mwanaume ila neno sahihi ni KUOANA.
 
Back
Top Bottom