Kuoga kila siku kiafya ni sawa?

Miss Natafuta

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2015
Posts
27,031
Reaction score
49,928
Watu wengi tunaishi tu kwa mazoea nadhani,

Jana kuna jirani yangu ni mkorea alikuwa anasafiri leo asubuhi usiku alikuja kuniomba msaada flani akanikuta naoga ilikuwa saa tano usiku hivi. Leo asubuhi akaja kuniaga tena aniachie maua yake niyanyeshee akanikuta naoga akashangaa akaniuliza mbona naoga oga sana nikamuambia mbona kawaida tu akasema sio vizuri kiafya kuoga mara kwa mara yeye akasema anaoga mara mbili au tatu kwa week.

Kidogo nizimie ila ukimuangalia yupo tu vizuri. Najua watoto wadogo ndo hawaogeshwi mara kwa mara japo kibongobongo watoto wetu wachanga wanaogeshwa sana tu asubuhi na mapema kanapigwa maji mchana, jioni muda wa kulala katoto kanapigwa maji kama amphibia vile chura sio samaki.

Ila watu wazima tunaoga kila siku hadi mara tatu naomba tujadili kiutu uzima kuna haja ya kuoga kila siku? Faida zake na hasara zake.

Asanteni.
 
Mimi huwa naoga kabla ya kufyatuana na baada ya kufyatuana yaani mara tatu au nne kwa wiki
 
Kiafya mara 1 kwa ck ila inategemea na kazi ya mtu, au mkoa, mfano kama dar joto sana so kwa jasho lile inabidi hata mara 2 kwa ck,

But pia kazi anayofanya mtu kama ni mizunguko sana mara 2 au moja co mbaya
 
Nilipo kuwa mkoa wangu ule wenye baridi nilikuwa naoga siku ya Jumapili tu ya kila wiki.Yaani ukiwa mwanahesabu vizuri nilikuwa naoga mara 4 tu kwa mwezi.
 
Kuoga kunafanya mwili kuwa Safi,kunaondoa some of bacteria n Smell's
 
hata wachina wanahisia hizo kwamba eti unaharibu ngozi
 
Kuna muda kuoga kunakuwa kama dawa hasa ukiwa na uchovu au kutojisikia vizuri.
Unaweza kujikuta hujielewielewi lakini ukioga tu unachangamka.
Kuoga mara kwa mara hufanya mwili ujisikie vizuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…