Miss Natafuta
JF-Expert Member
- Sep 16, 2015
- 27,031
- 49,928
Watu wengi tunaishi tu kwa mazoea nadhani,
Jana kuna jirani yangu ni mkorea alikuwa anasafiri leo asubuhi usiku alikuja kuniomba msaada flani akanikuta naoga ilikuwa saa tano usiku hivi. Leo asubuhi akaja kuniaga tena aniachie maua yake niyanyeshee akanikuta naoga akashangaa akaniuliza mbona naoga oga sana nikamuambia mbona kawaida tu akasema sio vizuri kiafya kuoga mara kwa mara yeye akasema anaoga mara mbili au tatu kwa week.
Kidogo nizimie ila ukimuangalia yupo tu vizuri. Najua watoto wadogo ndo hawaogeshwi mara kwa mara japo kibongobongo watoto wetu wachanga wanaogeshwa sana tu asubuhi na mapema kanapigwa maji mchana, jioni muda wa kulala katoto kanapigwa maji kama amphibia vile chura sio samaki.
Ila watu wazima tunaoga kila siku hadi mara tatu naomba tujadili kiutu uzima kuna haja ya kuoga kila siku? Faida zake na hasara zake.
Asanteni.