Kuogopa kununua Toyota Prius ni ushamba au umasikini

Katika kuhakikisha Prius inakwenda kupendwa zaidi. Mwaka huu wamefanya full body re design na gari ya Prius inaweza kwenda hadi kilometre 30 kwa litre.

Imetoka ya trim mbili.
Moja ni prius ya kawaida ambayo ni 1.8L Hybrid yenye 196HP sawa na nguvu ya toyot Brevis ya 1JZ.

Ya pili ni Prius Prime ambayo itakuwa na 2.0L Hybrid engine inayozalisha 221HP. Hii ni zaidi ya nguvu ya Toyota Crown Athlete za 4GR.

 
Dah bora hii mpya kali, sio ile ya zamani front kama chura alf jamaa analazimisha watu waipende
 
Kaka hyo 2000cc ndo balaaa 221hp mbona hatariiiiii
 
Kitu kikali
 
Haikawii utaiona imepaki mahali flani mjini pale pembeni ya ukuta wa shivacom 😄
Halafu bei yake kwa mpya haifiki hata usd 30, 000 ukiweka na shipping ndio labda inakuwa hio. Ukiweka na kodi kandamizi za kibongo inaweza kuwa around $45,000 almost million 105,000,000 hivi ila unachana makaratasi mwenyewe una uhakika gari haitokusumbua kwa miaka 10 ya mwanzo ya matumizi.
 

Mil 100 kwa ajili ya hivi vigari vya kwenda sokoni?! Hujanishawishi bado
 
Hili gari zuri sana japo sipendi shape yake ya mbele ila nazikubali sana.
Nshaziona kwenye movie nyingi za kimarekani.
Pia bongo napishana nazo kadhaa. Ila kila nikisoma sifa zake nakubali kuwa ni gari nzuri na miaka ya nyuma kabla tesla kuvuma, niliwahi soma kwamba ni hybrid ambayo ilijipatia umaarufu wa kutosha
 

Gari nzuri saana nmeziona nyingi sana USA [emoji631]

hizi zinatumika kama taxi kule pamoja na Camry
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…