Kuogopa kununua Toyota Prius ni ushamba au umasikini

ukiachana na kuogopa umeme ,design ya hii gari pia haijakaa sawa ndio maana watu wengi hawaichangamkii sana
 
Ni kweli design ya hii gari haivutii kabisa, ila hizi bei za mafuta zinakoelekea, design ya gari itakuwa anasa when it comes to buying hii gari au honda insight
Kweli mkuu. Naona Aqua na Honda fit hybrid zinanunuliwa sana na wazambia. Nadhani wameshtukia mchezo.
 
Gari yoyote ambayo haielewani na testa ya fundi shabani na wenzake sinunui maana ndo nikipata tatizo nawapigia hata nikiwa wapi wanakuja.
 
Mkuu naomba kujua kama una uelewa wa Nissan X Trail T32 hybrid ya mwaka 2015.
Hybrid battery zake zinauzwa bei gani hapa Tanzania?
 
Sasa wewe unajua Watanzania ni maskini alafu unashauri watu, wanunue magari ya kwenye lami tu huku kifulu haifiki, ukienda kijijini kinyanambo, uiache iringa mjini.
Sisi tunapiga ndege mmoja kwa jiwe mmoja.
Hahahahahah haitoboi kwa godoro na milima ya chekanao hahahah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…