Kuogopa Maandamano ni ushamba na kutojiamini, tuliandamana miaka ya Mwalimu!

Kuogopa Maandamano ni ushamba na kutojiamini, tuliandamana miaka ya Mwalimu!

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
18,653
Reaction score
31,010
Kwa miaka hii ya karibuni, tena wakati huu ambapo tunajiita Demokrasia imeongezeka, inashangaza watu kuogopa maandamano.
Nimemsikiliza Wazira juzi kwenye luninga , nikajua huyu ni mshamba mwingine tu.

Miaka ya Mwalimu, kwanza tukiwa Praimari, yalitokea maandamano makubwa sana kuunga Azimio la Arusha mjini Dar es salaam mwaka 1967.
1784791804677.png

Maandamano hayo yalikuwa ya akina Baba Kabwela na vijana wa Tanu Youth League. Na waliishia Ikulu kuonana na Mwalimu kabisaa!

Maanadano mradi ni ya amani, ni sehemu ya kuonyesha hisia za wananchi juu ya jambo lolote nchini liwe la kisiasa au kijamii.

Nikiwa sekondari Pugu 1975, hali ya chakula shuleni ilikuwa mbaya sana. tena sana.
Wanafunzi tukaandamana kilometa zaidi ya 10 , tena tulipita mbele ya kambi ya FFU-Polisi pale Ukonga, bila tatizo lolote.
Maandamano yalienda hadi kwa Mkuu wa Mkoa Mama Bernadeta Kunambi(Mungu amrehemu), ambaye baada ya kusikia kilio chetu aliwasilisha matatizo serikalini na jambo likashughulikiwa MARA MOJA.
Mama Kunambi akituona kama watoto wake akaagiza mabasi ya UDA yaturudishe hadi Pugu, iliyokuwa mapori wakati huo.

Hiyo ndiyo ilikuwa Serikali ya watu, serikali ya Watanzania.
Maandamano yote yanapaswa kuwa na sababu, zieleweke wazi na yasindikizwe na polisi ili vibaka na waleta fujo wadhibitiwe.

Sasa leo maandamano ni uhaini?
Ni jambo la kishamba sana kutoweza kuelewa kuwa lazima patakuwepo maandamano hasi(kupinga Jambo) au maandamano chanya (kuunga mkono jambo), alimradi yanafanyika kwa amani.
Hii ndiyo sehemu yake demokrasia duniani pote.

Lakini uongozi sehemu yoyote ile, iwe serikali au Taasisi yoyote, isipojiamini, inaona maandamano ni tamko la kuwaondoa ofisini.
Huu ni ushamba wa madaraka.

NB: Mimi ni CCM damu damu!
 
CCM imeshatoka kwenye reli kitambo sana. You probably won’t live to see a fully rehabbed CCM.
 
Back
Top Bottom