Kuolewa kuitwa heshima au kutokua heshima ni mtu binafsi mwenyewe anavyo fafanua...
Kitu cha msingi labda tuangalie kua jamii inamchukkulia vipi dada/mama ambae hajaolewa...
Yule ambae hajaolewa... na kawahi olewa huishi kwa amani zaidi katika maisha yake, sijui
ni kwanini ila wataona kua' kua divorced/widowed/telekezwa at least inam paint kua
anafaa na kawahi kua wife wa mtu...
Yule ambae hajaolewa kabisa ni shida saaana jamii kumchukulia positively hasa kama
umri umeenda saana, hata kama yeye personally hataki maisha ya ndoa (ambao ki ukweli
ni rare...) wataishia kumzushia alikua anachagua saana wachumba sasa kakosa wote,
au alikua mhuni saana, au kua sio wife material na maneno kibao... yeye anaweza asisikie
but ukweli ni kua majority inamchukulia hivyo...
Kwa kujibu kutumia jamii yetu ya Tanzania hii... kuolewa ni heshima mbele ya macho
ya jamii, na huheshimiwa kuliko yule ambae hajaolewa... tuache haya mambo ya mjini
na kuangalia jamii kama jamii yetu ya TZ... Hivyo bora hata uolewe uachike kuliko kutoolewa kabisa.
Number ya wadada wanokataa kua kuolewa sio heshima unakuta mara nyingi ni wale
walisha olewa alafu mwanaume akawa hafai... au bado she is young... au kweli
ni mkubwa lakini karidhika na maisha yake ingawa lazima kuna pressure from
family na jamii hapa na pale..