Sasa weweee. . .
Kama unaona kuwa mzuri ndio utiiwe sio haki kwasababu unatakiwa kufanya kitu kwanza kwanini unataka utiiwe kwanza ndio uwe mzuri kwa mwenzako? Maana nayo ni ile ile, unataka YEYE afanye kitu (kukutii) ndio umwie mzuri. Awe mtiifu UWE MZURI (hiyo ni kanuni yako) ,AWE MZURI nimtii (hiyo ni yangu).
Swala la kusema mtu kuitwa boyfriend/mume tu inatosha kutiiwa sijui kuheshimiwa inaweza ikaapply kwa wengine bali sio kwangu. Kwangu hayo ni majina pekee hata sanamu inaweza ikapewa. Heshima inapatikana kwenye matendo na sio majina. Siwezi kumtii mwanaume anaelewa na kurudi kushusha mtusi na kipondo juu, anaetoka nje ya mahusiano na asiyeniheshimu. Kwa maana nyingine mimi sio limbukeni wala siko tayari kuwa kwaajili ya ntu yeyote yule. The same goes for me, sitegemei wala sitaki mwanaume anipende kama simtendei haki na akifanya hivyo ntamwona ni limbukeni. Ndio maana kuna wanaume wanaonewa sana na wake/wapenzi wao. . .kwasababu wamekubali kuwa malimbukeni.