Gily Gru
JF-Expert Member
- Jul 4, 2016
- 8,632
- 23,673
Wasalaam wana JF
Unakuta mwanaume alikuwa na mke na wanaishi pamoja pika pakua. Ikatokea kuhitilafiana na wakachukua maamuzi ya kutalikiana kila mtu aende kumi zake. Baada ya kila mmoja kusukuma gurudumu la mahusiano na watu wengine huko waliko mwisho mahusiano yakatika kikomo pia.
Unakuta wanarudi kwenye ndoa zao za awali kurudisha mapenzi na kuamua kuishi kinyumba tena. Hivi wanaume wenzangu, unapataje ujasiri wa kumrudisha kinyumba mke wako mliyetalikiana. Kwa kweli hili swala hata kwa tafakuri zangu naona sitoweza ashakumu sio matusi kuyarudia matapishi yangu niliyoyatapika, ni ngumu mno kwangu. Si kwa ubaya, ila nashangazwa na ujasiri wa watu wanaofanya hivi, tena unakuta mwanamke anarudi na matunda ya ile ndoa aliyoachika (watoto wawili au watatu😬) na unafurahia kabisa kuitwa baba😬😬
Siwezi semea wanawake wana hisia gani kuhusu hili swala, labds wao wemyewe wafunguke. Ila kama mwanaume rijali mwenye familia na watoto wawili; Mangi kutoka Rombo hata nyinywe mbege pipa mbili maamuzi yangu hayatabadilika asilani.