Kuolewa ukaachika au kutoolewa kabisa, kipi bora?

Duuh,, umenena.
 
Hakuna kilicho bora
Kuachika ni aibu na ni sifa mbaya
Kutoolewa kabisa nalo ni tatizo

Dadaa,
Hapana kwa kweli, kuachika usichukulie kuwa ni kubaya. Sio wote huwa wana tatizo. Kwani huyo bwana hawezi kuwa ndo tatizo?? Pia, yawezekana sio kiungo chako huyo hivyo hata ungempikia kungu halainiki, mwisho utamwacha tu la sivyo ufwe kwa vidonda vya tumbo.
Pengine ni kunguru, hafugiki. Utaendelea kukaa hapo ili iweje?? Ni mbaya tu kama wewe ndo kunguru
 
Kwenye maisha hamna kitu bora au cha afadhali ...inategemea umekutana na situation gan na kwa kipindi gani...
 
Kwani kutosoma kabisa au ukasoma ukafeli unafikiri nini bora!?Aliyejaribu akafeli anaujuzi zaidi kuliko ambae hajajaribu kabisa!
here in Tz the edu. is so simple like that if you score 0 then simply you bashite, the game over.
 
Hakuna kilicho bora
Kuachika ni aibu na ni sifa mbaya
Kutoolewa kabisa nalo ni tatizo
Kama ulizaliwa na unaishi ili uolewe yaani ghamira kuu ya maisha yako ni kuolewa.. mchango wako ni sahihi..
Mm nafikir watu wakionana na hawaishi kwa amani ktk ndoa na hawana furaha kama walivyotarajia ni bora wakaachana....
Na pia kama mtu haoni anayemfaa ili kuishinae ktk ndoa bora akakaa tu ivoivo..
Huku kujifanya mnashida mno za kuolewa kunachangia sana kunyanyasika... ningeshauri familia ziwaandae watoto wote ( kike na kiume) vizur ili waweze kuhimili maisha bila kuwa tegemezi..
Hakuna fedhea kuachana na mtu, wala hakuna fedhea kutoambatana na mtu..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…