Kuomba kuoneshwa kipindi chako katika TV au kusikilizwa redioni

entry

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2018
Posts
286
Reaction score
539
Wakuu kwema, naomba tujadili hili tuweze kuongeza maarifa.

Hivi inawezekana kuomba kuonyesha kipindi chako katika kituo fulani cha TV au kusikilizwa redioni?

Kama jibu ndiyo;

1. Gharama kwa kukadiria inaweza kuwa shilingi ngapi? Najua ngumu ila kwa makadilio tu tupate mwanga.

2. Utahitaji uwe na kibali kutoka mamlaka yeyote ile ya umiliki wa hicho kipindi?

3. Mmiliki anaweza kupata faida yeyote kwa kumiliki hiko kipindi?

4. Je, kati ya redio na TV ipi ina gharama nafuu za uendeshaji (gharama nafuu za kuendesha kipindi).

Kutoka katika mawazo yangu na kwa watu wanaonizunguka, nasikia kipindi kama Mkasi ilikuwa inamilikiwa na mtu siyo kituo kinachoonyesha, kwahiyo inawezekana kumiliki kipindi.

Kuhusu swala la faida inaweza kupatikana endapo kampuni ikataka kutangaza bidhaa au huduma zake. Radio ina watu wengi na rahisi kufikia watu tofauti na TV, lakini suala la gharama sifahamu.

Naomba kuwasilisha.
 
Kulipa wewe ngumu sana, lazima utafute sponsor. Maana mfano Tangazo tu la dakika 1 kwenye TV unakuta mamilion.
Sasa hapo unatakiwa uandae proposal uwapelekee masponsa kama Voda, Coca, etc.

Maswali yako:
1. Gharama ngumu kujua kutegemea na TV na muda na maudhui. Maana vingine bure (mfano Misa za jumapili, Msikitini) ila mfano Chereko ile ilikua (sijui kama bado ipo) TBC unarusha harusi yako ilikua mil , 2 kasoro, kama sijakosea.

2. TCRA lazima wahusike ila pia wenye TV wataangalia (wahariri) kama mahudhui yako hayavunji sheria.

3. Mmiliki wa iko kipindi (wewe) utapata faida through sponsors na kama kitakuja kupendwa zaidi baadhi ya matangazo muda wa kipindi unaweza kua unapata mgao kidogo. Ingawa hapa sina uzoefu.

4. Hiyo ipo wazi mbona. Radio cheap. TV nuksi.
 
Tcra watahusika katika vibali ama nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…