Akili Unazo!
JF-Expert Member
- Feb 18, 2009
- 3,930
- 4,912
Wakuu hivi kuna haja yakuomba msamaha pale unapoambia kuwa umekosa na wewe huoni kama umefanya hilo kosa au ni bora kukaa kimya kwa kuepusha shari? au ni lazima unapoambia kuwa umekosa hata kama kosa ni la upande wa pili ukubali kuepusha shari na kuomba msamaha??
...'mwanga mpe mwanao amlee',
Tell me about it my brother....'mwanga mpe mwanao amlee', wewe mwombe msamaha, akishaanza kujichekesha mwulize kwani ulimkosea nini?!
Pride ni kitu mbaya sana wanajamii.
Tell me about it my brother.
na je mtu anayekukosea na anajua kabisa hapa nimecheza rough lakini haombi msamaha wala nini tena ndo kwanza anaact kama vile hakuna kilichotokea (hata kama anajua wewe una hasira) utamwelewaje?
Tell me about it my brother.
na je mtu anayekukosea na anajua kabisa hapa nimecheza rough lakini haombi msamaha wala nini tena ndo kwanza anaact kama vile hakuna kilichotokea (hata kama anajua wewe una hasira) utamwelewaje?
...swadakta! unakumbuka kindergatten/primary school na hata boarding school (enzi za u -njuka aka form 1) kulikuwa na wale bullies? yaani almuradi tu akuchokoze mpigane? How did you cope with that?
..tactics zile zile zilizoku shape utotoni ndio zitumie ukubwani, kwani unajua faida na hasara zake. Kama 'vagi' litakunasua kwenye makucha yake, ruksa! ...kama ukimpuuzia ajione mjinga ndio suluhisho, deal with it!
...binafsi nakushauri mpuuzie. Hawa spouses wetu kuna wengine ni spoiled brats tangia huko mwa wazazi wao, kwetu wanakuja kuhitimisha tu. Mpuuzie.. mwache ajigalagaze machangani, apige mayoe hata akitaka ajikojolee, mwache hivyo hivyo na 'nepi' yake!
... Ignore him!
................. Duh kweli ukubw adawa. Aksante kaka somo zuri
Ila ukumbuke kitu kimoja mpenzi alichosema Mbu hapo juu kina ukomo wake, sio ku-ignore kila kitu hadi unajikuta kaburini kisa unapuuzia tu eti kwasababu kuna siku ataacha, watu wengine ni kama taahira ukipuuzia na yeye ndio anakaza mwendo. Mimi kwa mtazamo wangu weka mchanganuo ni mambo gani ya ku-ignore na ni yapi ya kuangalia kwa undani na kuyachukulia action
Aksante Sipo umenielimisha sana inawezekana huwa nakosea mfano akichelewa kurudi au asiporudi kabisa nyumbani usiku (na kama ulishawahi kusema na bado mwenzio hajirekebishi) huwa nategemea atoe taarifa kuwa atachelewa au hata akichelewa basi apige simu aseme yuko wapo (ili tu atutoe wasiwasi sie tulioko nyumbani) sasa asipofanya lolote na bado akarudi late na bado asiseme kitu kuexplain wala kujitetea yaani aact kama hakuna alilofanya ---- nilidhani kupuuzia katika hili si sawa au nakosea?
Mpenzi MJ1 hakika ili sio la kupuuzia kwa sababu mumeo/mpenzio anaweza kuona hali ile haikukeri kwahiyo ataendelea nayo wakati wewe roho inataka kukutoka kwakuwa hujui anachelewa wapi na anakuwa anafanya nini. Ni muhimu kuuliza na kupata majibu. Ndio maana nikasema ku-ignore sana na kila jambo si vyema sana kwani watu tumetofautiana
..... Aksante Sipo. Mie nadhani nina roho ya ajabu au ndo kiburi ninachosemwa nacho kila siku. Kama nilishakuwa namwuliza kila mara akichelewa na yeye habadiliki na pengine ukimsema leo klama karudi saa nane kesho atarudi saa kumi (kama si dharau ni nini?).
.... Aksante Sipo.Mumy MJ1 kama mtu karudi saa nane usiku leo ukamuuliza halafu kesho akarudi saa tisa usiku, sintosita kusema kuwa ni dharau na dalili za wazi za kwisha kwa mapenzi. Hata kama uliuliza kwa approach gani lakini kuchelewa nyumbani mpaka saa nane ni kosa hata kama umtu alikuwa kwenye biashara kwahiyo lazima utoe taarifa mapema na kuomba radhi. Watu wasitake kuleta habari za akina Ihucha bwana. Mapenzi ni kujaliana bwana na sio kuumizana jamani.