MwanajamiiOne
Platinum Member
- Jul 24, 2008
- 10,470
- 6,580
Mie naona kuomba msamaha ni poa tu, kama umemkosea mwenzako kwa nini usiombe msamaha... hii ndiyo kuanzaisha resentment kibao migogoro ikaanza na taking each other for granted..... juzi Mr. nikiendesha gari...mara nishaambiwa nipack gari kando oh sijui ataendesha yeye. Ala!!!! nilinuna mpaka akaomba msamaha kwani mie mtoto!!!!! tena ikawa sitaki kumuona.
Si hiyo ya kunyamaza as if nothing happened?
... unaomba msamaha wa nini wakati umekusudia kutenda...
Aksante Mbu. Sikuwa nimeiona
.... Nigeieni basi na mimi hii bahati? maana mie weza nuna hadi jua likashuka na msamaha usiombwe hata kama kakosa yeye....... yaani nimechoka kabisa
pole sista.... hivi bado hujatatua yale mambo?? wanaume wa aina hiyo wanaudhi sana.. sijui huwa ndiko kuonyehsa ushujaa ama hawataki kuonekana kuwa na weakness... jamni kuomba msamaha isnt a sign of weakness but of respect, love and thats what real gentlemen do! mmm pole aisee sasa umemuaje dadangu? I feel your pain as a sista!
......... dada na visa kila kiukicha vinaibuika- nadhani ni yale ya akufukuzaye hakwambii toka.
...swadakta! unakumbuka kindergatten/primary school na hata boarding school (enzi za u -njuka aka form 1) kulikuwa na wale bullies? yaani almuradi tu akuchokoze mpigane? How did you cope with that?
..tactics zile zile zilizoku shape utotoni ndio zitumie ukubwani, kwani unajua faida na hasara zake. Kama 'vagi' litakunasua kwenye makucha yake, ruksa! ...kama ukimpuuzia ajione mjinga ndio suluhisho, deal with it!
...binafsi nakushauri mpuuzie. Hawa spouses wetu kuna wengine ni spoiled brats tangia huko mwa wazazi wao, kwetu wanakuja kuhitimisha tu. Mpuuzie.. mwache ajigalagaze machangani, apige mayoe hata akitaka ajikojolee, mwache hivyo hivyo na 'nepi' yake!
... Ignore him!
Mkuu Mbu, nakuunga mkono kabisa yote unayoyasema lakini wengine ni Bullies ukiamua kumignore hapo ndiyo ataongeza jingine sasa kwamba unamdharau kwa kutomsikiliza anayoyasema na kuongeza ugomvi na kuwa mkubwa zaidi na yeye kudhani kwamba unamdharau kwa sababu kuna mtu anayekuvimbisha kichwa anakufundisha kiburi etc, kumbe wala hakuna mtu kama huyo bali umechoshwa na kelele zisizo na kichwa wala miguu ambazo hutokea karibu kila siku iendayo kwa mungu.
Kuomba msamaha kwa maoni yangu si kitu cha ajabu lakini inabidi iwe ni 2 way traffic wanaume nao wawe tayari kusema 'samahani' pale wanapogundua kwamba wamekosea na si mwanamke tu ndiyo awe muomba msamaha kila anapokosea vinginevyo itafikia wakati na yeye ataamua kuomba msamaha sasa basi, hata anapojua fika kwamba amekosea.
Wanaume wengine wanajisikia sana kiasi ambcho kutamka neno 'samahani' ni kujishusha hadhi yao kama wanaume hivyo hata wanapojua fika kwamba wamekosea hawawezi kulitamka neno hilo. Hili ni kosa kubwa kama mnataka kujenga uhusiano wa kuheshimiana kati yenu maana hakuna binadamu ambaye yuko perfect na asiyefanya makosa na pia makosa madogo madogo tunaweza kabisa kuyamezea badala ya kutaka kuanzisha kasheshe kila unapoona kosa hata kama halina athari yoyote katika uhusiano wenu.
We Za10!WoS na BAK mnaleta uBeijing. Mwanamme akosehi bwana na hakuna sababu ya kuomba msamaha.
We Za10!
Unataka kusema nini sasa? yaani mtu aseme kile ambacho hakipo au siyo ukweli anaoamini just because atakutana na backlash kama hivi?
Usidanganye wenzio.Tena mtu kama wewe utakuta mwepesiii kuomba msamaha.Halafu hapa unawadanganya wenzio wakomae tu!!
Ndugu yangu...
nakupongeza sana kwa kutokuwa biased.Hujapendelea wanaume wenzio kama ambavyo ingeweza kufanywa na mwanaume mwingine kulinda ego.
Ni watu kama wewe mtakaobadilisha hali ya unyanyasaji katika mahusiano.Im sure kama kuna bullies humu wanasoma mchango kama huu basi wataona haya na kufikiria kubadilika.Ungegombea ubunge nakuhakikishia ningekupigia kampeni na ungepata kura za wanawake wote kiulainiiiiii.
WoS na BAK mnaleta uBeijing. Mwanamme akosehi bwana na hakuna sababu ya kuomba msamaha.
Mwanaume hakosei kwa sababu tuko perfect! Wenye makosa siku zote ni wanawake! Halafu mke akiamua kuondoka ndiyo mtu anaanza kusikitika, Ooohhh! I made a big mistake I am still in love with my wife...