Kuna hadithi moja ya Kichina, ambayo inasema zimwi mlawatu ana sura ya kutisha, ili kudanganya watu, hujipamba kama mrembo. Marekani inajitahidi kutengana na China katika mambo ya kiuchumi na kibiashara. Baada ya kupingwa kwa kauli moja na jumuiya ya kimataifa, ilibadilisha sura yake na kusema inataka kuondoa tu hatari zinazosababishwa na China. Kitendo hicho ni sawa na hadithi ya zimwi mlawatu.
Katika miaka ya hivi karibuni, Marekani imezidi kuwa na “wasiwasi” kuhusu China, na imefanya mambo mengi ili kuzuia maendeleo ya China. Katika sekta ya uchumi na biashara, Marekani imewekea China vikwazo vingi, na zaidi ya hayo, imezichochea nchi nyingine haswa zile zilizoendelea, kuchukua hatua kama hiyo dhidi ya China. Hata hivyo, China ni nchi ya pili kwa uchumi duniani, nchi kubwa zaidi ya kiviwanda, na mshirika mkuu wa biashara wa zaidi ya nchi 140 duniani. Kuvunja uhusiano wa kiuchumi na kibiashara na China kwa kweli kutadhuru sana maslahi ya nchi hizo. Ripoti iliyotolewa na taasisi moja ya utafiti ya Ulaya inakadiria kwamba, ikiwa Ujerumani itatengana na China kiuchumi na kibiashara, pato lake la ndani la kila mwaka litashuka kwa asilimia 2. Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alisema wazi kwamba Umoja wa Ulaya na China zinapaswa kufanya juhudi kwa pamoja ili kutoingia kwenye mtego wa kutengana. Hata nchini Marekani, watu wengi, haswa wale wa sekta za uchumi na biashara, wanapinga msimamo wa serikali yao dhidi ya China. Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tesla ya Marekani Elon Musk, amesema maslahi ya Marekani na China yamefungamana, kama mapacha walioungana.
Baada ya kushindwa kushawishi pande nyingine kutengana na China moja kwa moja katika mambo ya uchumi na biashara, serikali ya Marekani imetafuta njia nyingine mbadala. Baada ya kutangaza “kuondoa hatari” dhidi ya China kwa mara ya kwanza kwenye mkutano wa kilele wa G7, hivi karibuni Marekani iliitisha mkutano wa mawaziri wa nchi za bahari ya Hindi na Pasifiki, na mkutano wa biashara kati ya Marekani na Umoja wa Ulaya, ili kutetea “kuondoa hatari” dhidi ya China. Marekani inadai China imeleta hatari nyingi kwa uchumi wa nchi zilizoendelea, ili kuvutia nchi nyingine kupingana na China katika mambo ya uchumi na biashara.
Kitendo cha Marekani kimeamsha umakini wa jumuiya ya kimataifa. Naibu Waziri Mkuu wa Singapore Wong Xun Choi amesema, kauli ya “kuondoa hatari” dhidi ya China badala ya “kutengana na China” pia itasababisha kugawanyika kwa uchumi wa dunia, hali ambayo italeta changamoto kubwa kwa biashara na uwekezaji duniani.
Uundaji na maendeleo ya minyororo ya kimataifa ya uzalishaji na ugavi ni matokeo ya soko. “Kutengana” au kinachodaiwa kuwa “kuondoa hatari” dhidi ya China, sio tu kwamba kutazidhuru nchi zinazohusika, lakini pia kutaleta hatari kubwa kwa utulivu wa minyororo ya kimataifa ya uzalishaji na ugavi, na pia kusababisha uharibifu wa kudumu kwa uchumi wa dunia. Nchi zinazohusika zinapaswa kugundua hila ya “kujipamba kwa zimwi mlawatu”, na kurudi kwenye biashara huria na uchumi unaofungua mlango.