Kuondoa na kurudisha sh. 100 kwenye bei ya mafuta nani awajibike?

Kuondoa na kurudisha sh. 100 kwenye bei ya mafuta nani awajibike?

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Rais Mama Samia alirejesha tozo ya Sh.100 iliyokuwa imetolewa kwenye mafuta ya petrol, dizeli na mafuta ya taa ni nani alikosea kuitoa na ni nani kati ya wafuatao ajitafakari kati ya Waziri wa nishati na waziri wa fedha na afanye hivyo lini ili iwe fundisho kwa wengine?

Kama Ndugai ilijitafakari kwa kutaka kulikosesha taifa pesa kwa njia ya mikopo kwanini hawa waliolikosesha pesa taifa kwa njia ya tozo washindwe kujitafakari?

Tuepuke kufumbia macho double standards ili tusikwame huko mbele ya safari, Mama Samia ameonyesha kuwa yuko serious na nchi hii, tusimchukulie poa na tusije tukasababisha kampeni zake huko mbele.

Serikali yote ya CCM na Wabunge wake wote, akiwemo huyo mnafiki Luhaga Mpina.
Kosa ambalo halikuadhibiwa hujirudia. Dhamira ya kuiondoa 100 bila shaka ilikuwa njema lakini utaratibu wa kuiondoa uliruka hatua mbalimbali muhimu, nani hakufanya nini na nani alifanya nini kwenye hili. Mheshimiwa Ndugai alituonyesha njia wa namna kiongozi mtoa maamuzi anapoteleza anavyotakiwa kufanya na kufanyiwa. Bussiness as usual lazima ikome,
 
Hakika umenena vizuri sn
Tujenge utamaduni mpya wa kupongezana na kulaumiana kwenye maslahi ya taifa bila kujali ni nani kafanya vizuri au amekosea. Hivyo ndivyo wenzetu wanaofanya vizuri kwenye uchumi wao wanavyofanya. Waafrika wanatabia ya kupigia makofi kila mtu kila jambo analofanya kiongozi, ilimradi awe wa Chama chao. Nadhani Rais Samia anataka kuugeuza utamaduni huu. Kama kiongozi kwake Kumetokea shida kubwa ya kizembe awajibike mwenyewe au awajibishwe, kila mtu kuanzia kwa Rais lazima ajue uongozi wa nchi sio ajira yake bali utumishi wa watu.
 
Kwa hii katiba mbovu siyo rahisi
 
Tozo kwenye mafuta ya shilingi 100 kwa kila lita 1 ya mafuta ni ndogo sana, angalau ingekuwa 300 kwa kila lita ya mafuta.
 
Back
Top Bottom