Kuondoa Option ya kuangalia salio la Data Bundle Airtel ni kuweka mazingira ya kutuibia

Kuondoa Option ya kuangalia salio la Data Bundle Airtel ni kuweka mazingira ya kutuibia

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2014
Posts
7,926
Reaction score
17,030
Kama sikosei ni week ya 3 hii napojiunga kifurushi cha data kupitia Airtel sipati option ya kufahamu nmetumia au kubakiwa na data kiasi gani.

Hapa wametengeneza mazingira ya kumwibia mteja. Ili ije tokea suddenly death. Ukishtuka tu wanakwambia umeshatumia takriban asilimia 90 wakati unasoma hiyo text unaaambiwa salio limeisha.

Sasa huu si wizi? Airtel maisha yamekuwa magumu kwetu sote.si ninyi peke yenu. Huu mchezo mnaofanya si mzuri unaweza kutufanya nasi tuanze kufikiria michezo mingine then tukaingizana hasara.

Tupeni Menu yenye Option ya kuangalia salio la data lililobaki. Mkiendelea hivi naelekea kufungua kesi mahakamani ya Wizi kwenye Data zangu.
 
Na Halotel wamefanya hivyo kwenye dakka. Huwezi kuona salio. Kama una namba ya TCRA niwekee hapa please
 
Menu zipo nyingi bwashee,dial *148*88#ok,kisha chagua namba 8/salio.
 
Ndo maana hata simu zetu hizi janja zina option mbili za Sim Card. Why unang'ang'ania mtandao huo huo wakati imejazana kibao mzee?
Wahame kwa mda uwape sababu ya kuboresha.
Shida ya wateja huwa hawaijui vizuri nguvu yao na ndipo wanapopigwa.
Mtandao mmoja umeung'ang'ania kama ndoa Katoliki.
 
Hawaoneshi salio la Data
Nikweli kabisa mkuu hawaonyeshi.mimi ninatobo la kupata 1gb kila siku,nimeangalia salio la data awakuleta wameleta la vocha(airtime) lakini mb zimo na nazitumia.
Duh,,hapa sasa kuna harufu ya kupigwa watu.
 
Mbona ipo, unaweza kuangalia salio bila shida yoyote.
Anacholalamikia mtoa mada ni kwamba, ukiambiwa umetumia %90 ya bando, muda huo huo kabla haujaingia kuangalia salio kwenye menu tayari wanakwambia kifurushi kimeisha.

Maana yake ni kwamba mf: 90% ya gb1 ni mb 900, zinazokuwa zimebaki ni 100 mb.

Sasa 100 mb zinatumika ndani ya sekunde 1?

Hiyo ndiyo mantiki hasa ya mtoa mada.
 
Screenshot_20201019-151051~2.png


Angalieni wenyewe. Bado wamenificha salio la Data.

*149*99*10*1#

*149*99# haifanyi kazi?


Menu zipo nyingi bwashee,dial *148*88#ok,kisha chagua namba 8/salio.

ubarikiwe mkuu

Mbona mm naangalia vizuri tu kila siku.
 
Back
Top Bottom