Kuondoa trafiki wenye vitambi barabarani ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu; Haiwezekani bila kubadili mfumo

Kuondoa trafiki wenye vitambi barabarani ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu; Haiwezekani bila kubadili mfumo

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Nitaeleza kwa kifupi Sana!
Maana nafahamu watu wengi wanapenda mijadala ya pombe na umbea kuliko kuchangia mijadala ya haki na katiba!
JE; KITAMBI NI KOSA LA ASKARI AU LA MFUMO WA KAZI?

Watu wengi huwa wanashabikia mambo bila kuangalia kanuni za kazi zikoje!?
kazi ya Utrafiki siyo nyepesi Kama watu wanavyoichukulia.

Ni kazi yenye maelekezo kulingana na sheria za inchi na kanuni zilizopo! mfano; Sheria ya usalama barabarani etc
Ni kazi inayojumuisha mambo mengi ikiwemo ulinzi, kuzuia magendo, usalama wa watumia barabara, mawasiliano ya njia, na kusaidia kusimamia maelekezo ya mamlaka zingine. mfano (TRA ,Misitu, bahari et)

Kwahiyo ili Askali afae kuwa Traffic Officer Ni lazima Ahudhurie mafunzo maalum (kozi maalum) ili aweze kusimamia hayo ipasavyo!

Kwa mujibu wa Sheria zetu Tanzania (Road Traffic act), Traffic ni officer Anaruhusiwa kukagua chombo chochote Cha usafili barabarani hata Kama ni toroli pasipo kuogopa hadhi au cheo Cha mtu anaeikiendesha!

Ndiyo maana Traffic Ni kikosi kamili ndani ya Jeshi la polisi!

Ili Askari uweze kumbadilishia kikosi kuwa Traffic! Shuruti aende mafunzo ya miezi mitatu!

MASWALI

SWALI; Kama Traffic mwenye kitambi utamuondoa kisa kitambi, UNA UHAKIKA GANI KAMA HUYO ANAEKUJA HATOPATA KITAMBI?

Je, MIFUMO iliyompa KITAMBI huyu hakiwezi kumpa KITAMBI mwingine ajaye?

Je, Trafiki officer anawajibishwa na nani awapo barabarani endapo atambambikia mtu makosa?

Je, Ni mda gani Trafiki Anaruhusiwa kumshikilia dreva wawapo barabarani pasipo kumpotezea mda ili asishawishike kutoa rushwa kwa hofu ya kupotezewa mda?

Je, Ni mambo gani Trafiki wa kawaida haruhusiwi kukagulia barabarani bila kuwepo kwa VEHICLE OFFICER!

Je, Upi Ni utaratibu maalum wa kukagua,? au ni maamuzi binafsi ya Trafiki atakavyoamua kukagua ili kutafta kosa? N.K

KITAMBI NI MFUMO, TUBADILI MFUMO KWANZA VITAMBI VITATOKA VYENYEWE!
 
kwa kweli inaonesha jeshi hakuna mazoez baada ya mafunzo kabisa watazame askari baada ya mwaka au miaka utapata majibu wangeweka mfumo ambao kila bada ya mwaka angalau miezi miwili waludi kwenye kwata angalau
 
Mbona wachezaji kwenye Vilabu hawapati Vitambi, simply tu Ukiota Kitambi Jeshini kazi huna au unakatwa Mshahara tuone kama watalea hizo Ndulla zao. Ni fedhea sana kuvaa kwanda za JESHI ukiwa na "Mimba uzembe" shit kabisa.
 
hata umuweke Nani mimba ataipata kwa hela ya kiwi na supu
 
Mbona wachezaji kwenye Vilabu hawapati Vitambi, simply tu Ukiota Kitambi Jeshini kazi huna au unakatwa Mshahara tuone kama watalea hizo Ndulla zao. Ni fedhea sana kuvaa kwanda za JESHI ukiwa na "Mimba uzembe" shit kabisa.
waende gwaride halafu magendo yasafilishwe!🙄
 
kwa kweli inaonesha jeshi hakuna mazoez baada ya mafunzo kabisa watazame askari baada ya mwaka au miaka utapata majibu wangeweka mfumo ambao kila bada ya mwaka angalau miezi miwili waludi kwenye kwata angalau
Kazi anazofanya askari ni zoezi tosha sana, kitambi kikifika mda wake kinaota tu hata upige mazoezi kitaonekana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom