matunduizi
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 7,968
- 19,368
Nimetafakari nikakumbuka story ya jamaa waliokuwa wanamkimbiza mwizi ila hawamjui (hawana target). Kufika sehemu wakaanza kuulizana mwizi yuko wapi kila mtu hata mimi sijui.
Kuondoka kwa JPM kumewavua nguo wapinzani.
1: Imethibitika huwa wanapinga watu na sio mfumo uliopo dhidi ya mfumo mbadala wanaouamini.
2: Sasa hivi kama wamepigwa butwaa wanashindwa wanzie wapi. Wampinge mama au washambulie Marehemu. Wapowapo tu bila dira.
3: Hawana dai moja lenye consistency ambalo hata kama chama tawala kibadilishe mtawala wao wapigekelele yenye kiwango hichohicho. Ni kama watu wanaofukuza upepo, unakoelekea nak wanakimbizia huko.
4: Sasa hivi ndio ilikuwa fursa ya kutushawishi wananchi maana mambo mengi yako neutral. Ila naona kama wanaviziavizia kutafuta viudhaifu wapate pa kuanzia kufanya mihadhara.
5: Wanaichukia CCM wakati wanamsifia Rais wa CCM. Haijulikani wakati uliopita walikuwa wanampinga rais au taasisi nzima iliyokuwa inatawala maana wanayemsifu ndiye mshauri pia wa yaliyopita.
Wapinzani mmeacha ombwe kubwa sana, akitokea mtu mwenye akili na rasilimali fedha na ushawishi anaweza kuanzisha chama bora msimu huu kinachoweza kufuta Chadema, CUF, ACT n.k maana wameshindwa kujua kuna mapinduzi makubwa sana ya kimtazamo wa kisiasa hadi kwa mtanzania asiyejua kitu sasa kuliko miaka 6 iliyopita. CCM wanajitahidi kuwa agile wakinyumbuka kila kukicha wakati wenzao wako rigid wakiishi kwa kitegemea tuhuma na tetesi na sio mipango.
Yangu ni hayo tu.