St. Paka Mweusi
JF-Expert Member
- Sep 3, 2010
- 7,956
- 5,149
Nawasalimu kwa heshima na taadhima wakuu. Alfajiri ya leo mida ya saa kumi na nusu nilitoka ili nifanye mazoezi ya kukimbia kwa nusu saa. Kilichonishangaza ni kuona mgongo wa mnyama mkubwa kuliko mbwa na anamkaribia simba akitembea katika majani marefu. Sikuweza kuona kichwa chake wala mwisho wa mkia wake. Na alikuwa akielekea upande mwingine tofauti na nilipokua naenda mimi. Tukio hilo lilodumu takriban sekunde sita akapotelea kwenye nyasi. Kwa utaalamu wangu wa kuwafahamu wanyama na tabia zao nilishawishika kuamini kuwa yule alikuwa ni simba mtoto au aina nyingine ya paka mkubwa. Bahati mbaya sikuwa na simu ya kuchukua japo picha. Akawa katoweka. Na hili jambo nimelishuhudia leo hapa Dar maeneo ya Goba takriban mita 500 toka stendi ya Goba mwisho njia ya kuelekea Makongo. Sasa swali ninalojiuliza ni je kuna mtu yoyote hapa ambaye alishashuhudia au kusikia tetesi za kuonekana kwa paka wakubwa katika jiji la Dar na viunga vyake?