Kuongeza thamani ya gari lako!

Kuongeza thamani ya gari lako!

No Escape

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2016
Posts
6,663
Reaction score
7,785
Baada ya kuhakikisha gari lako lipo makini hasa upande wa kiufundi kwa maana ya safari salama,kuna haja ya kuliweka gari yako kuliweka katika hali ya kimtazamo wa kipekee! Yaani lisionekane kama hulitaki wabongo wakiona hivyo hawakawii kukwambia uwauzie...Mimi binafsi gari naliona km wife material,kulipendezesha sioni gharama sana vitu km Bampers,carriers wheel covers sunvisors n.k. Ila yale mataa mataa ya pembeni sishauri. Naomba huu uzi uwe maalum tushauriane jinsi ya kufanya magari yetu yawe na mwonekano wa kipekee Ina raha yake jamani....Sio mtu unamiliki Harrier Hakuna tofauti na kirikuu.
 
Ni kweli kabisa hata mm pia nathamini gari nnazo tumia, kwanza afya ya gari. Running condition, spare, matunzo yani service isiwe ya kuunga unga. Genuine filters oil nzuri na bora, uijue gari yako vizuri yani mf. Unaeza ukawa unatumia model flani ila ziko various like 2.0L or 2.5L hyo inamaana na ina impact kubwa. Tunza kias kwamba hata siku yakuuza huuzi sababu bovu ila Una badili gari tu, na pia sometimes hauuzi ila watu wanasumbua kulinnua.

Likiwa vyema hapo ndo unakuja vitu vichache vya kulifanya liwe zuri, kutunza rangi, kutokuwa rough kwenye uendeshaji, mziki mzuri, air freshener, na unaeza enda mbal zaidi kuchange paint code, rims, kama fan wa sports car kama mimi utaongeza performance pia kwenye engine kufanya modification, kuweka spoiler nzuri carbon fibre siyo ilimrad tu spoiler, lakini bila kuzidisha. Maana dah kuna watu gari ina makorokocho mpaka mtu unasema ukipewa lift hupandi [emoji23][emoji23][emoji23] gari inabeba vitu mpaka inakuwa nzito.

Na kupenda gari ni hobby pia siyo kila mtu anaweza, ina gharimu inabidi uwe tayari kuspend. Of which nipo tayari miaka yote nafanya. At least mtu awe mtunzaji tu, asi skip service. Ina cost sana mwishoni engine ikifika au ukikosea kitu.
Free advice on car care.
 
Katika vitu nachukia ni Mipambo miiingi kwenye gari mpaka linageuka kuwa kama katuni. Gari lina urembo mpaka linakera mweeeeeeee. Yaani gari inapigwa drill mashine mpaka juu ya bonnet kisa tu urembo huu ni USHAMBA tubuana, be Gengleman hayo mambo ya Urembourembo ni ufala. Anyway hata sisi binadam saa, pete 6 vidoleni, cheni 8 shingoni, simu 6 mkononi, meno nane ya mbele yana dhahabu..Hakyani hata salamu yangu sikupi naokuona bwege fulani tu.
Be simple Man.....
 
Customisation ya gari inatakiwa iwe simple na ya kuvutia kwa kila mtu na isiyochosha macho ya watu mapema. ..
Kwa mfano mimi binafsi napenda Rim kali, mziki wa wastani mzuri....si yale matwita utafikiri muuza karanga anachezesha kile kikopo cha mchanga...,
rear spoiler nzuri na gari iwe na rangi moja inayovutia..

Si gari inakuwa na mataa ya rangi rangi nje utafikiri ni kasino inayotembea ...khaaa..
 
Katika vitu nachukia ni Mipambo miiingi kwenye gari mpaka linageuka kuwa kama katuni. Gari lina urembo mpaka linakera mweeeeeeee. Yaani gari inapigwa drill mashine mpaka juu ya bonnet kisa tu urembo huu ni USHAMBA tubuana, be Gengleman hayo mambo ya Urembourembo ni ufala. Anyway hata sisi binadam saa, pete 6 vidoleni, cheni 8 shingoni, simu 6 mkononi, meno nane ya mbele yana dhahabu..Hakyani hata salamu yangu sikupi naokuona bwege fulani tu.
Be simple Man.....
WEWE MIMI KABISA
 
Rim matata ikiwa na low profile tire, mziki wa wastani na mara nyingi ni ule unaokuja na gari kwani hupenda kuagiza gari ambayo ina sound system kamili.Gari iwe safi muda mwingi na huosha mwenyewe mara mbili kwa wiki mbali na ninazopeleka car wash... gari iwe inanukia pmj na kufuata taratibu zote za itunzaji wa jiko lake, huepuka sana mikono mingi kwenye uendeshaji,
 
Back
Top Bottom