Kuongezeka kwa Matamasha ni faida kwa Wasanii au ndio Mwisho wa Mipaka yao ya kazi..?

Kuongezeka kwa Matamasha ni faida kwa Wasanii au ndio Mwisho wa Mipaka yao ya kazi..?

mayowela

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2014
Posts
2,125
Reaction score
1,753
kwa sasa kiwanda cha burudani kimechangamka na kimechangamshwa na uhasama wa Media houses mbalimbali za hapa nyumbani,

kila media sasa ina Tamasha lake, pia kuingiza mkono kwenye matamasha mengine kama Udhamini wa matamasha yanayoandaliwa na Makampuni makubwa ya simu, vinywaji baadhi yao hupewa tenda za kusimamia,

Kuna matamasha kadhaa,
Fiesta chini ya Mdhamini mtandao wa simu Tigo, Precision Air nk na Clouds media
Mizki Mnene chini ya EFM na wazamini BULL CONDOM, BIKO nk
Wasafi festival chini ya WASAFI Media wazamini Startimes, Airtz, nk
Kulishawahi kuwa na Jembeka Festival Mwanza Chini Ya Jembe fm mzamini Vodacom

Sasa kuna baadhi ya wasanii inaonekana wakiingia mkataba kwenye tamasha moja hawawezi kuingia mkataba kufanya shoo tamasha lingine hata kama ratiba inamruhusu huko nikujifunga kitanzi,
Baadhi huogopa akienda kufanya shoo kule huku ni kama rotation ya mziki wake utapungua tumeshuhudia hayo,
kuna ambao tayari tumeyaona, Young Killer, Barka the Prince, JUX, MADEE

Lakini jingine kama msanii ni Balozi wa Vodacom inakuwaje hawezi kufanya shoo kwenye tamasha ambalo mzamini ni TIGO, Kujifunga nako huko,

Ninachokiona kuna wasanii wajasili ambao watapiga pesa endapo watasaini mikataba au kuhitajika kwenye kila tamasha, na wengine hawawezi fanya hivo wakihofia vipaji vyao kufa na pia kupokonywa ubalozi,

Akili mkichwa wajitambue wawe na wanasheria wasaini mikataba vizuri ili isiwabane kwenye fursa kama hizo laa sivyo watajiwekea mipaka kwenye kazi zao.

wasalaam.
 
jibu ni moja tu.


ni nafasi ya wasanii kuokoteza jasho lao.
leo tunaenda kwa kiba na watu wake,kesho kwa kondeboy na watu wake,keshokutwa kwa mond na watu wake.finally watu wanapata nguvu hata ya kutoka nje.

naamini katika hilo.
 
jibu ni moja tu.


ni nafasi ya wasanii kuokoteza jasho lao.
leo tunaenda kwa kiba na watu wake,kesho kwa kondeboy na watu wake,keshokutwa kwa mond na watu wake.finally watu wanapata nguvu hata ya kutoka nje.

naamini katika hilo.
safi sana, sema inabidi wajitambue waache uteam na wasaini mikataba ya show kwa umakini
 
Back
Top Bottom