Baba Joseph17
JF-Expert Member
- Jul 15, 2013
- 9,517
- 9,762
Sasa! Kama hata kliniki mtoto wako anapelekwa, ina maana hata muda wa kuandaa lishe ya mtoto na kujua afya yake hufuatilii. Chukua muda wa kuandaa lishe ya mwanao, unategemea 'dadaa' ndo akufanyie kila kitu, nae pia anapenda kuboresha afya yake.
unataka mtoto wa tipwatipwa....?je ni wakike au wakiume?
Ni wakiume, wasiwasi wangu ni kwa nini hajaongezeka uzito kwa muda wa mwezi 1 na nusu ili hali watoto wengine aliozaliwa nao kipindi kimoja wanaongezka kiasi.
Ni wakiume, wasiwasi wangu ni kwa nini hajaongezeka uzito kwa muda wa mwezi 1 na nusu ili hali watoto wengine aliozaliwa nao kipindi kimoja wanaongezka kiasi.
Wasiwasi wako tu, kwa umri wa mtoto na uzito alionao ni sawa kabisa. Swali la msingi kwanini humpeleki mtoto clinic wewe mwenyewe ukizingatia umri wa mtoto bado sana kumuachia mtu mwingine ampeleke? Jitahidi kumpeleka mtoto clinic wewe mwenyewe huko utaongea na nurse/dr kujua maendeleo ya mtoto wako
Alipelekwa na mama yake, mie sikuwepo siku hiyo huwa tuna mpeleka nikiwa nyumbani.