Kuota kwa kokwa la tatu ndani ya korodani!

Kuota kwa kokwa la tatu ndani ya korodani!

Fikrazangu

Member
Joined
Dec 31, 2017
Posts
15
Reaction score
25
Habari zenu wana JF?! Nina tatizo la kiafya nalo ni kuota kwa kokwa la tatu ndani ya korodani. Kama tunavyofahamu, korodani huwa na kokwa mbili. Hivi karibuni nimeanza kuhisi kuota kwa kokwa la tatu upande wa kushoto. Kokwa hili nikiliminya kidogo linaleta maumivu. Nimejaribu kugoogle na majibu niliyopata ni kwamba kitaalamu hii inaitwa "Polyorchidism" na tovuti nyingi zinaeleza kwamba ni tatizo ambalo hutokea kwa nadra sana na kwamba haijafahamika chanzo chake ni nini! Nimeona niwashirikishe hili ili kama kuna mtu ameshaexperience tatizo kama hili au kama kuna mtaalamu wa afya anieleze lina athari gani kiafya.
 
Habari zenu wana JF?!

Nina tatizo la kiafya nalo ni kuota kwa kokwa la tatu ndani ya korodani. Kama tunavyofahamu, korodani huwa na kokwa mbili. Hivi karibuni nimeanza kuhisi kuota kwa kokwa la tatu upande wa kushoto.

Kokwa hili nikiliminya kidogo linaleta maumivu. Nimejaribu kugoogle na majibu niliyopata ni kwamba kitaalamu hii inaitwa "Polyorchidism" na tovuti nyingi zinaeleza kwamba ni tatizo ambalo hutokea kwa nadra sana na kwamba haijafahamika chanzo chake ni nini! Nimeona niwashirikishe hili ili kama kuna mtu ameshaexperience tatizo kama hili au kama kuna mtaalamu wa afya anieleze lina athari gani kiafya.
 
Pole sana ngoja wajuz waje, ila nakushauri nenda hospitali ,yawezekana unatakiwa ufanyiwe upasuaji
 
Du kaka hiyo sio dalili nzuri sana ,na huwezi kusema ni kokwa ya 3 bila kufanya vipimo, Mara nyingi anomalies zote za viungo mtu anazaliwa nazo na zinakuwa with time ila yakutokea ukubwani ni new growth.
Ushauri wahi mapema hospital wakakupime ,watch out for testicular tumors ambapo dalili yake ni uvimbe kwenye pumbu ambao unaweza zania ni kende nyingine.
 
Mkuu hiyo ni normal condition na hutokea baadhi ya males.

Cha kukupongeza ni kwa kujiongeza mpaka umeijua hiyo condition uliyonayo.

Sasa cha muhimu zaidi ni kufika kwa mtaalamu wa afya ili aweze kukufanyia check up ili kuona kama kuna shida yoyote.

Kama hakuna dalili yoyote ya cancer au maradhi mengine huwa hakuna tiba inayofanyika kwakuwa ni condition isiyo na madhara hata katika fertility.

Cha muhimu uwe unafanya check ups hata mara moja kila mwaka kuona maendeleo yakoje na kuweza ku monitor kama kuna growth yoyote ya cancer cells.
 
mkuu hiyo ni normal condition but kwa vile umesema ukiminya inakuletea maumivu ni muhimu kuwahi hospital kwa ajili ya matibabu .
matibabu :
ni kwa njia ya Upasuaji

side effect ni kupungua uwezo wa pulling
 
Du kaka hiyo sio dalili nzuri sana ,na huwezi kusema ni kokwa ya 3 bila kufanya vipimo, Mara nyingi anomalies zote za viungo mtu anazaliwa nazo na zinakuwa with time ila yakutokea ukubwani ni new growth.
Ushauri wahi mapema hospital wakakupime ,watch out for testicular tumors ambapo dalili yake ni uvimbe kwenye pumbu ambao unaweza zania ni kende nyingine.
NJE YA MADA
Hivi wale bongo movies wanapoandika "watch out part 2" huwa wanamaanisha nini?Lugha hizi!😂😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom