Fikrazangu
Member
- Dec 31, 2017
- 15
- 25
Habari zenu wana JF?! Nina tatizo la kiafya nalo ni kuota kwa kokwa la tatu ndani ya korodani. Kama tunavyofahamu, korodani huwa na kokwa mbili. Hivi karibuni nimeanza kuhisi kuota kwa kokwa la tatu upande wa kushoto. Kokwa hili nikiliminya kidogo linaleta maumivu. Nimejaribu kugoogle na majibu niliyopata ni kwamba kitaalamu hii inaitwa "Polyorchidism" na tovuti nyingi zinaeleza kwamba ni tatizo ambalo hutokea kwa nadra sana na kwamba haijafahamika chanzo chake ni nini! Nimeona niwashirikishe hili ili kama kuna mtu ameshaexperience tatizo kama hili au kama kuna mtaalamu wa afya anieleze lina athari gani kiafya.