Kuota uko unapiga na paper halafu kitu kinakupanikisha

kwa vile brother Mshana yuko hapa, usiwaze sana ndugu yangu mambo yatakua sawa. Zingatia tu huo ushauri wake hajawai feli hua anasema ukweli cku zote.
 
Wote mnao ota ndoto mko darasan na ilihali mmesha labda mlimaliza shule au mliacha , muoneni mshana kwani sio ndoto za kawaida , pia kama unaota wewe ni mtoto wakati una nywele za ukubwani muone mshanajr
 
miongoni mwa ndoto zangu hadi leo hii, sijui tatizo ni nini
 
Bora wewe paper la form 6. Mimi mpaka paper la darasa la saba tena shule ile ile halafu unakuta kuna somo sijasoma kabisa
mm form 4,yaaan kinachonishangaza kwamba kuna kuwa na somo moja sijasoma, bali kila siku miaka yote
 
hii ndoto ilikuwa inanitoke kipindi nipo final year nilikuwa na stress hatari mara nyingine nilikuwa naota napiga UE kichwani zero au naota niko O level kwenye paper alafu sijasoma nikishituka najisemea ohh hakuna paper bora, nilipomaliza zangu final year sijawahi kupata tena ndoto hizo.
 
Ndoto sio lazima iwe na ukweli

Mie mara kadhaa huwa naota naacha kuvuta bangi akati kiuhalisia sijawahi hata kuwaza kuacha
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
dah mkuu nilijua nipo peke yangu,hakuna ndoto nazichukia kama hizo unajikuta unaota hujajiandaa kitu half muda wa kuingia kwenye pepa unakaribia dah yani unajikuta unapanic kinyama huko ndotoni [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Jaribu kujichunguza kwa upande wangu most of the time nikiota hivyo kuna jambo litatokea ambalo nitarudi nyuma kimaendeleo .
 
Nimetoka kuota ndoto ya kudaiwa vicoba😂😂 wakati sijawahi ingia kicoba cha aina yoyote Wala Sina deni popote, sometimes ndoto hukosea njia ilmradi ikusumbue tu
 
Kumbe waotaji wa hizi ndoto tupo wengi🤔
Nilidhani ni mimi peke yangu ndie nayeota 😂😂.
Juzi kati nimeota nipo kwenye ratiba ya mtihani wa mwisho wa kidato cha sita necta cha ajabu nawaona wahuni wenzangu niliomaliza nao form four 🤔
 

Someone trying kurudsha malengo yako unayopanga yasifanikiwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…