Kupambana na uhalifu kihalifu hakukubaliki

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Uhalifu hauna msamaha wala kusingizio. Haipo sababu inayoweza kuuhalalisha. Uhalifu utabakia kuwa hivyo bila kujali ni nani afanyaye uhalifu huo.

"Kumwua mtu kwa makusudi hakukubaliki."

Ni muhimu kuwakemea kwa nguvu zote ikiwamo kuwachukulia hatua kali polisi wauwao watuhumiwa kwa makusudi kinyume cha sheria.



Kuwekeza nguvu za kutosha katika kuwaadibisha wahalifu wote bila kujali majina yao au hata vyeo vyao, kunapaswa kuwa ndiyo mwelekeo wetu.

Shime waungwana haya huwa hayaji kama mvua.

"Mwendo na ukawe kukemea vikali na kupigania uwajibikaji kwa vitendo."

Tuungane kuupinga uhalifu, yakiwamo ya "uharamia wa polisi" na "mauaji yao kinyume cha sheria."

Beberu akiyaita "police brutality" and "extra judicial killings."

NInakazia: Uhalifu haukubaliki.
 
Wewe unaonesha unafadhili ujambazi na vikundi vya uporaji, hivyo nakuomba uache ni hatari kwako.

Mimi ukinambia jambazi anatakiwa kuishi nashangaa sana na pengine hujawahi kupotezewa mpendwa wako na hao majambazi ,mimi kila nikikumbuka madhila ya hao unaowatetea mpaka kuacha watoto yatima naumia sana.
 
Thread za aina hii zinakosa wachangiaji lakini ikija inayomuhusu Magufuli kila panya atatoka kwenye tundu lake.

Utashangaa wanazungumzia ubaya wa Magufuli kuzuia mikutano ya siasa na utekaji kinyume cha sheria, lakini hawaoni umuhimu kuwaasa polisi wasijichukulie sheria mkononi kinyume na taratibu kuhusu panyarodi.

Hawa viumbe wana upendeleo, wao wanadai haki kwa yule wasiempenda aliemnyima haki yake wanayempenda, lakini haki kwa wasio na uhusiano nao wa aina yoyote kwao haina maana, hata mlalamikaji asipopewa ni sawa tu, double standard.
 

Kwani jambazi anayestahili kuishi hapa ni yupi?



Kama ni kwa mtazamo kama wako tu, kwa nini jambazi na mfadhili wao usiwe wewe ndugu?

Hata wale wafanya biashara wa ifakara ilikuwa hivi hivi ana kwa ana na majambazi yasiyokuwa na huruma.

Mark my words: police brutality haikubaliki!
 

Usijali kuhusu wachangiaji. Ujingani mada za wachangiaji ni zile zenye hisia ngono na kubeza ma single mother.

Kuna alinizukia kihasara hasara bila shaka akidhani kila mtu anahusudisha upumbavu wake.

Yuko salama anakostahili.
 
Usijali kuhusu wachangiaji. Ujingani mada za wachangiaji ni zile zenye hisia ngono na kubeza ma single mother.

Kuna alinizukia kihasara hasara bila shaka akidhani kila mtu anahusudisha upumbavu wake.

Yuko salama anakostahili.
Mtalia sana na kusaga meno
 
Police brutality haikubaliki.
 
Je jambazi yupi kakamatwa?
 
Kwani jambazi anayestahili kuishi hapa ni yupi?

View attachment 2369608

Kama ni kwa mtazamo kama wako tu, kwa jambazi na mfadhili wao usiwe wewe ndugu?
Kaka unajiabisha sana kufanya utetezi wa wahuni hata Marekani yenyewe ambayo ndio tunaamini haki za binadamu zinazingatiwa lakini linapokuja suala la kudhibiti Ugaidi ,gaidi anauliwa mchana peupe na hakuna anayehoji haki za binadamu wala haki ya mtuhumiwa ila aibu naona Mimi mnapata wapi nguvu ya kutetea majambazi wasiotakiwa kuishi?
 
Nashauri polisi kabla ya kuua panya road wahakikishe wanae/ wanao muua/ waua ni panya road kweli ili kutokomeza panya road wote wa kweli na sio ambao hawana hatia.

Note: anae ua kwa upanga na yeye anapaswa kuuawa kwa upanga, sihitaji kusikia kwa sasa neno la kipumbavu liitwalo haki za binadamu kwa muuaji especially hawa panya road, majambazi , watekaji, wabakaji , watu wasio julikana n.k .
 

1. Police wanahakiksha vipi huyu ni panya road kweli kweli?
2. Zipo kesi nyingi na zingine hata ziko mahakamani leo, watuhumiwa wa ujambazi ni polisi.
3. Upo ushahidi wa kutosha kuwa watu wasiojulikana ni polisi.
4. Nk nk.

Tarime walifika na kuchukua watu kwenda kuwauwa ambao jamii inakataa kuwa si majambazi.



Dhana ya polisi jamii Iko wapi?
 
Naomba usome mara ya pili nilicho andika,usipo elewa au usipo taka kuelewa utakuwa na tatizo ndani ya kichwa chako.
 

Wapi tunapotetea majambazi.

Unaelewa maana ya kufanya uhalifu?

Unaweza kuhalalisha kufanya uhalifu?

Zingatia ni msimamo wetu kuwa uhalifu haukubaliki.

Kwa nini hauoni aibu wewe kutetea uhalifu?
 
Ukisema wanakutukana, Kuna wapuuzi wanashabikia Polis wanavyoua raia eti Panyaroad, Polisi wa Tanza-nia ni genge la Wahalifu. Take it or not,
 
Naomba usome mara ya pili nilicho andika,usipo elewa au usipo taka kuelewa utakuwa na tatizo ndani ya kichwa chako.

Nimesoma mara kadhaa kabla ya kukujibu kwa ufasaha kabisa kuwa polisi hana namna ya kumjua panya road 100% kwa sababu yeye si malaika.

Nikakufahamisha kuwa kuna polisi majambazi wengi tu na wengine hata leo korokoloni.

Nikakufahamisha utambulisho wa wasiojulikana ambao bila ya shaka unaujua.

Nikakwambia uzingatie hata polisi jamii kutoheshimiwa. Kumbuka wakazi wa Ifakara walikataa kata kata. Wafanya biashara wale hawakuwa majambazi.

Yote haya kukuitisha uone umuhimu wa kufuata sheria kwa sababu hayupo malaika kwa usalama wetu sote.

Tatizo liko wapi hapo?

Tafadhali rejea kujridhisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…