Kupambana na watu wasiojulikana: Ukija kukamatwa na polisi bila uniform na hajaambatana na kiongozi wa eneo husika piga firimbi, kusanya nzi

Mimi nilikamatwa wiki jana kwenye kituo kidogo cha polisi. Wakasema wanasubiri afande wao mwenye V mbili, nikasubiri mpaka jioni nikaona hawaji. Nikaomba kwenda haja nikatoroka. Kesi yenyewe ya kuhisiwa tu
 
Umeeleza vizuri sana ! 🙌🙏
 
Juju lipo Mzee !
Ni Ubaya Ubwela kwa kwenda mbele !
 
Arusha huko sijui tengeru, kuna watu wameshamvuliwa...na raia
Walidhani ni watekaji watoto
Wamechezea mapanga,kipondo
Walipaki gari raia walikuwa hawawaelewi....kumbe ni watu familia walikuwa na mambo yao tu...
Juzi tu nimetoka kumcmnt humu kuwa sahv raia wataanza kujjlinda wajuavyo wao na lazima action watakazo chukua zitakuwa na mabalaa tu
Tutazidi kuona na kusikia visa

Ova
 
Hatari sana !
Mambo yakifikia out of control itabidi walioyaanzisha wajitokeze hadharani na kutubu !!
Mabalaa katika Nchi yanaanzaga hivi hivi kama utani !

Tuombe Mungu tusifike huko 🙏🙏
 
Muhimu sana kujilinda wakati huu, usikae kizembe.

Usipokee hovyo hovyo namba usizo zijua.

Ukiona jumbe zisizo eleweka wataarifu ndugu na jamaa wa karibu.

Usiwaamini sana watu wa pembeni wengine ndio wachoma ramani yako.

Nawakumbusha tena usikubali kamwe mpumbavu mmoja ama wawili kukuteka kwenye karandiga yao kama mzoga pambana uwezavyo.

Wao si ndio wahuni basi nasi twende nao kihuni hivyo hivyo.
 
Hatari sana !
Mambo yakifikia out of control itabidi walioyaanzisha wajitokeze hadharani na kutubu !!
Mabalaa katika Nchi yanaanzaga hivi hivi kama utani !

Tuombe Mungu tusifike huko 🙏🙏
Sahvi ni kukaa kwa tahadhari
Ukienda sehemu huna mgeni kaa
Mguu sawa maana lolote linaweza tokea
Ukienda sehemu kwa wale wenye magari wanapaki tu bila kueleweka nao wakae mguu sawa
Lolote linaweza tokea,
Nlikuwa nawasikiliza hawa jamaa waliyokuwa arusha wanasema sjui walipaki gari,mara wakawaona watoto wakawa wanawaita wanawapa pipi balaa ndiyo likaanzia hapo,

Ova
 
Maelezo na ushauri mzuri sana!!

Kule Dodoma wameanza kutupiga na kutuchomea kwenye nyumba
 
Hatari sana !
 
Tangu utawala wa Magufuli watanzania wengi wamekuwa wakilalamika kutekwa kupotezwa na miili kuokotwa fukweni au porini kama ilivyotokea kwa Sativa na Dr. Ulimboka. Nimeamua kuwapa ushauri tu, kama hutaufuata basi tambua kuwa wakishakuteka hautarudi tena. Watakutupa kama mzoga wa mbwa.

Zingatia yafuatayo
1. Usimuamini askari yoyote. Ukiitwa kituoni kama sababu inaonekana ni kukusaidia chochote basi usiende hasa unapoitwa kwa kupigiwa simu.

2. Hakikisha number mpya usipokee hovyo hasa ikiwezekana block number zote ambazo hujazisevu kwenye simu yako. Hii itakusaidia maana hawatakupata kirahisi.

3. Wito wowote wa ghafla na rafiki yako bila mpangilio usiukubali.

4. Jilinde - Unajua kuwa police wanakutafuta basi jitahidi kujilinda.

Wanao tafutwa sana ni CHADEMA NA WAFUASI WAO na tambua kuwa CCM waliapa kuimaliza CHADEMA na polisi ni waajiriwa wa CCM na wao ni wanaccm kwahiyo ni juu yenu kudadavua.

JILINDENI MSIFE KIBOYA.

Pia soma=> Kupambana na watu wasiyojulikana: Ukija kukamatwa na polisi bila uniform na hajaambatana na kiongozi wa eneo husika piga firimbi, kusanya nzi
 
dah!
kumbe siku zote mlikua hamjilindi?
miljisahau au Imani ilikua kwa Mungu,

lakini sasa mnaamini ushirikina tu na kudanganyana namna za kijadi kujilinda, right? that is very wrong...

umaskini wa fikra na imani potofu ni utumwa mzito sana wa kifukara..

sikilizeni niwasanue, kwanza Muamini Mungu,

lakini pia,
vyombo vya ulinzi na usalama, muhalifu uwe na mawasiliano ama hauna, umejilinda ama vinginevyo. ukiwa muhalifu utatafutwa popote ulipo, utatiwa nguvuni na kisu au silaha za kijadi ulizonazo, na utawajibika kwa uhalifu wako mujibu wa sheria bila mbambamba yoyote, msidanganyane 🐒

Malaika Mkuu Gabriel atuondolee unyonge na hofu zisizo na maana yoyote na atulinde na adui muovu sote, sasa na hata milele .
Amina
 
Daaaah! Unajidanganya kuwa wewe huu ushauri haukuhusu eeeeeeh?
Unaifahamu ile hadithi ya "MTEGO WA PANYA"?
 
Hii hoja unaichukulia poa? Watu wanapotea ni lazima tuwasanue, watapunguza kuilinda ccm na uovu wao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…