Kupambana na watu wasiojulikana: Ukija kukamatwa na polisi bila uniform na hajaambatana na kiongozi wa eneo husika piga firimbi, kusanya nzi

Kupambana na watu wasiojulikana: Ukija kukamatwa na polisi bila uniform na hajaambatana na kiongozi wa eneo husika piga firimbi, kusanya nzi

Wasiojulikana na polisi kwa nini mtaki kusema ukweli hapa jf. Jeshi likapanguliwa. Lugha za stshaa za nini.
Ujifunzi kuwa wakija ukatumia hizo mbinu wakishaona umewagundua kesi utakayopewa umeingilia majukumu yao.
Hayo ya kuja ndio yana takiwa kukemea na kuwekwa wazi.
 
Kwa ambao tumesikia wamechukuliwa hivi karibuni na hata nyuma kuna ambako umesikia walivunja mlango au walimfata mtu usiku? Hao waliokuwa wananchukuliwa kariakoo si ilikuwa mchana kweupe? Ndugu yake Boniface Jacob alichukuliwa usiku?
ndio maana nikasema kama ni mazingira ya jumuia inawezekana ila ktk mazingira ya watu wachache haiwezekani watakumaliza hapohapo
 
Tembea na kitu cha kujihami hata kama ni kakisu flani hivi kazuuri kaliko nolewa kama wembe sasa wakijichanganya hata kama watakudhibiti lakini kakisu na kelele kuna chochote waweza okoa, huwa sisahau yule mkurya sijui mjita anaitwa ZAKARIA wa kule mara alivamiwa na wasiojulikana Wakampora bastola wakamfunga kamba wakamtupia kwenye Noah wakaanza kuondoka nae wakamchinje kumbe jamaa alikuwa na bastola nyingine kule kwenye soksi mguuni ndipo akaichomoa ile bila wao kujua PUMBAAAAFU! akamfumua dereva kiuno gari ikapoteza mwelekeo akamfumua goti yule mwingine SHEEEEENZI! kisha akamfumua vyumbu (mapu+mbu) yule wa tatu ndo wakasema kwamba wao ni usalama asiwaue! Ndo pona ya zakaria na kama mnakumbuka vizuri nadhani tangu tukio la ZAKARIA huu upuuzi ulipungua sana.

Nasema hivi tembe hata na petroli kwenye bakuli au kinyesi na kama unayo ya tumboni we harishia mmoja wapo pumbaaaafu
 
1. Kuomba dua kila wakati na kila baada ya swala
2. Kuswali swala za usiku huku ukiomba dua
3. Kusoma Suratulfat-ha, Nnas, Falaq na Ikhalas mara 3 kila siku
4. Ayatul-Kurissiyu kila siku
Ukifanya hata aje nani kwa ubaya na wewe hakuoni
 
1. Kuomba dua kila wakati na kila baada ya swala
2. Kuswali swala za usiku huku ukiomba dua
3. Kusoma Suratulfat-ha, Nnas, Falaq na Ikhalas mara 3 kila siku
4. Ayatul-Kurissiyu kila siku
Ukifanya hata aje nani kwa ubaya na wewe hakuoni

Hata kama mkuu wa serikali ni mswalihina?
 
Wakuu kwema,

Watu wasiyojulikana siyo maneno mageni kwetu, na mambo haya yameanza kitambo kuanzia enzi za Kikwete na Ulimboka (kusoma tukio hilo zaidi hasa kwa Gen Z soma hapa - Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sanaaliyetekwa na watu wasiyojulikana na kukukwa ametupwa kwenye msitu akiwa ameteswa sana na kung'olewa meno.


Kadri awamu zilivyobadilika na ndivyo matukio haya yamezidi kuongezeka, na sasa wamekuja na mbinu mpya.

Wanakuja watu wanaojitambulisha kama polisi na kutaka kukukamata, lakini wanakuwa wamevalia kiraia yaani hawana gwanda za polisi, watakuonesha kitambulisho (lakini hivi hata vya mchongo vinapatikana), wakiwa pia na gari binafsi, nyingi ambazo zimekuwa zikihusika ni Noa nyeupe au nyeusi, au zile Cruza, lakini pia jamaa huibuka wenyewe wenyewe tu bila kiongozi wa husika.

Kuelewa zaidi haki yako pale polisi anapokuja kukukamata soma: Jua haki yako unapokamatwa na Polisi

Mfano wanakuja mtaani kwako lakini mjumbe wa eneo husika hana taarifa, au anafika sokoni lakini hawaambatani na uongozi wa soko.

Polisi wakishutumiwa kuhusika na matukio haya wanakana, kwamba waliofanya matukio hayo siyo polisi, wanauliza uongozi wa eneo hilo ulikuwepo? Walikuwa na uniform? Walitoa vitambulisho? Walikuja na gari ya polisi?

Ukiangalia ni kweli sababu hawaendi na utambulisho wowote kuwa wale ni polisi, ni tobo (loophole) tunalotakiwa kuliziba, huku polisi wakitoa matamko polisi akija kwa namna hiyo (bila utambulisho official) basi mtuhumiwa anatakiwa kukataa kukamatwa!

Pia soma: Sativa225 (Edgar Mwakabela) kijana maarufu kwa kukosoa serikali X apatikana, baada ya kutekwa na watu wasiojulikana

Hapa kwenye kukataa kukamatwa ndio kunaleta ka ugumu, maana tuambiane ukweli kuwadindishia wajeda labda na wewe mwenyewe uwe na msuli, vinginevyo unapigwa makofi mawili, unashikwa kwenye pindo ya suruali huyo ndio umeenda hivyo.

TUFANYAJE SASA KUKABILIANA NA HAWA JAMAA WANAOITWA WATU WASIYOJULIKANA?

Bila wananchi kushirikiana hatuwezi kushinda hili, inabidi tuwe na umoja kama tunavyoshadadia mambo ya kijinga.

Kwenye maandamano yanayoendelea Kenya ili mwandamaji aepuke kukamatwa ovyo walikuwa wanatembea na firimbi, akiona ameshindwa anaichomoa fastaa anaipuliza wenzake wanajaa kuhoji kuna nini, tuitumie njia njia hii.

~ Ukiona watu wanaojitambulisha kama polisi hawajavaa uniform zao, wana gari private na wakati mwingine hakuna plate number, na wala hawajaambatana na uongozi wa mtaa/eneo husika wanang'ang'ana kukuchukua usiende kizembe, puliza firimbi yako, puliza kwa nguvu zako zote kushutua watu wajae.

- Huna filimbi siyo kesi, piga kelele, yaani PIGA KELELE kwa nguvu zako zote mpaka watu wajae, hapa na wewe usiwe mzembe, sema hawa wanadai ni polisi lakini hawana uthibitisho kuwa wao ni polisi.

- Tutumie simu zetu vizuri, wakati jamaa aliyeshikwa anapayuka na kelele zake, wengine rekodini kila kitu, tupate sura zao, pamoja na usafiri waliokuja nao. Namba halisi ya gari huwa inaandikwa kwenye kioo cha gari pale mbele upande wa dereva kama sijakosea, maana kuna uwezekano mkubwa plate iliyotumika ni fake chukueni video na ya namba hizo. Wengine mko vizuri kwenye utaalamu wa mitandao ya kijamii, badala ya kurekodi kwenye simu yako ingia kwenye mtandao wowote wa kijamii na urushe tukio hilo live, amini nakwambia ni dk 0 tu litakuwa limeshasambaa nchi nzima na hao jamaa hawatochomoka.

- Wakati hayo yanaendelea wahojini watu hao ni kina nani na wanatoka wapi, kwa kiasi kikubwa ili kuua soo wataingia kwenye gari na kusepa ili wasitambulike zaidi, ikiwa watatoa silaha, ni muhimu kujilinda, wakifanikiwa kuondoka na jamaa walau tutakuwa na utambulisho wao wote kuanzia sura mpaka namba kamili za usajili.

Kufanya hivi itakuwa rahisi kuwatambua watu hawa wanaotekeleza matukio hayo, na tukiwabaini ni polisi, Jeshi la Polisi litatueleza vizuri kwanini wanashiriki kwenye mauaji ya raia.

Kama nilichokiweka kina manufaa sambaza ujumbe kwa ndugu na jamaa tushirikiane kukomesha watu hawa wasiyojulikana.
Umesema kweli sana!
 
Kawaida yangu ninapoiona hatari kwangu na kwako kijana wa Kitanzania inakuja hata kama wakati huo nilikuwa juu ya kifua cha shemeji yenu hakika nitamuacha na kuamka na kuishika simu na kuandika haraka maana najua wengi mtanisoma na kusikia wosia wangu.

Nafanya hivyo maana najua utamu ndoa yangu ni wangu ila umuhimu wa nyinyi kuwepo Duniani ni muhimu zaidi ya utamu huu. Nawapenda sana vijana wa Kibongolendi maana hata Mimi nilikuwa kijana ila mwaka huu tarehe 12/11/2024, nitauaga ujana maana ntatimba 40 yrs hii ni robo sijui ya Karne Mimi sijui.(nikosooeni).

Vijana wa Kibongolendi nawaaasa amkeni acheni "ubogenye" churukeni, pigeni tizi chezeni makalateeee kwa ajili ya kujilinda wenyewe maana mamlaka ya ulinzi Imerudishwa kwenu nyinyi wenyewe na sio kwa vyombo vyetu vya usalama(vimewabwaga, nyanyukeni jilindeni)

Nawasanua vijana wa Bongolend amkeni hali si shwali nchini Tanzania, Spika wa bunge anasema hakuna utekwaji Kuna "ukenywaji"(kama ujaelewa UTAELEWA baadae)😬😄😀🙏)

MAHAKAMA ambao ni mhimili nao unasema hauna uhakika kama polisi imemteka Soka na wenzake kwa hiyo haiwezi toa oda iwalete mahakamani inawapa muda usio na kikomo wafanye upelelezi hahaahahahahhhhaahha hii ni kesi ya kwanza hisiyo na time limit Dunian.

Vijana wa Bongolend amkeni amkeni amkeni mjilinde wenyewe, jilindeni wenyewe kama mnavyolinda sehemu zenu za sirini, jilindeni wenyewe kama ambavyo mnakufa njaa hamna ajira lakini hamsemi mpo kimya.

Jilindeni wenyewe kama mnavyoona anasa za viongozi wetu wa siasa lakini mpooo kimya kama mipompompoooooo!

Jilindeni wenyewe kama mnavyoona vijana wenzenu wanatekwa lakini nyinyi mpo kimnya kama MITOYOOO AU LIRE JOKERI LA NAPE alilopeleka Bungeni likaishia kumuita Mhe. Nape.😬😁😄😀.


Yote kwa yote nawasanua pamoja na kujilinda, kwa kuwa wanaotuteka inasemekana ni wasio JULIKANA na wanakuja na nguo za ndani walizo NUNUA kwa kukodi zetu Sasa tusikubali kamwe, kukamatwana hao Midori mpaka wavae shanga (yaani wavae Gwanda na kama wana gari iwe Difenda).

Kinyume chake pambana na mdori huyo mpaka kieleweke piga kelele za hela yooote kijana wa bongolendi hela huna, ajira huna hata sauti huna ya kupiga kelele😁😬😀😄

Piga kelele wasanue wajazie nziiii. Hao Midori noa panga weka kwa kyupi usikamatwe kizeeeeembe.

Good morning my fellow.
 
Mkuu hebu weka kile kisa cha Aliyekua mmiliki wa mabusi ya Zacharia mana najaribu kuweka nashindwa ila yule jamaa alijua kuwaweza watu wasiojulikana mana alipita na risasi za viuno kama hana akili ukitokea tu na mkaunda kaunda suti wako unazo ,ukijikuna tu unazo Zacharia alitoa somo kubwa sana kwa wale jamaa ipo siku yao tena
 
Tembea na silaha hata kama ni kakisu flani hivi kazuuri kaliko nolewa kama wembe sasa wakijichanganya hata kama watakudhibiti lakini kakisu na kelele kuna chochote waweza okoa, huwa sisahau yule mkurya sijui mjita anaitwa ZAKARIA wa kule mara alivamiwa na wasiojulikana Wakampora bastola wakamfunga kamba wakamtupia kwenye Noah wakaanza kuondoka nae wakamchinje kumbe jamaa alikuwa na bastola nyingine kule kwenye soksi mguuni ndipo akaichomoa ile bila wao kujua PUMBAAAAFU! akamfumua dereva kiuno gari ikapoteza mwelekeo akamfumua goti yule mwingine SHEEEEENZI! kisha akamfumua vyumbu (mapu+mbu) yule wa tatu ndo wakasema kwamba wao ni usalama asiwaue! Ndo pona ya zakaria na kama mnakumbuka vizuri nadhani tangu tukio la ZAKARIA huu upuuzi ulipungua sana.

Nasema hivi tembe hata na petroli kwenye bakuli au mavi na kama unayo ya tumboni we harishia mmoja wapo pumbaaaafu
aaah huyo mwamba alifanya vzr sana ingebidi angemuua ata mmoja wapo maana hawakua na nia nzuri
 
Siku za karibuni kumekuwa na mambo mabaya ya kutisha, mambo ya kishetani kabisa, watu kutekwa na wengine kupotezwa moja kwa moja.

Utekaji huo mara nyingi umehusishwa na Polisi au watu wa usalama wa Taifa. Na wananchi wengi wameamini hivyo kutokana na mazingira ya matukio. Baadhi ya watekaji walipoenda kuwateka watu walijitambulisha kuwa wao ni polisi, na kwamba walikuwa wanawachukua kuwapeleka vituo vya polisi, lakini watu hao waliotekwa hawakuonekana kwenye kituo chochote cha polisi.

Polisi kwa upande wao wamekataa katakata kuwa wao hawahusiki na utekaji watu.

Kwa hiyo ina maana watu wamekuwa wakitekwa na maharamia kwa kutumia jina la polisi, na polisi hawawajui watekaji. Kwa mazingira hayo, polisi hawawezi kutuhakikishia usalama wananchi, kwa vile hawawezi kuwepo kila mahali, hivyo yatubidi wananchi tushiriki kwenye ulinzi wetu na wa wananchi wenzetu. Kwa kufanya hivyo tutakuwa tunashirkiana kikamilifu na polisi kwenye ulinzi wa Taifa letu dhidi ya haya maharamia.

Kama kuna mtu yeyote anatakiwa kukamatwa na jeshi la polisi kwa tuhuma zozote zile, taratibu za kumkamata mtuhumiwa wa uhalifu zipo wazi. Miongoni mwa taratibu hizo, ni pamoja na:

1) Polisi atafika ofisi ya Serikali ya mtaa au kijiji kuujulisha uongozi wa kijiji au mtaa kuwa kuna mtuhumiwa anayeishi eneo hilo wamekuja kumkamata. Na uongozi wa mtaa au kijiji utaambatana na polisi kwenda nyumbani kwa mtuhumiwa.

2) Polisi watajitambulisha kwa mtuhumiwa, na wataeleza kuwa wamekuja kumkamata kwa tuhuma ambazo watazitaja.

3) Kama kutakuwa na upekuzi, mtuhumiwa atakuwa huru kumwita mtu yeyote kuwa shuhuda wa upekuzi.

4) Mtuhumiwa akiwa mikononi mwa polisi ana haki ya kuwasiliana na ndugu zake au wakili wake na kumjulisha kuwa amekamatwa, anapelekwa kituo cha Polisi.

Hivyo basi:

1) wananchi tuwe macho na tuwe makini, usikubali kuondoka na watu ambao wamejitambulisha tu kuwa ni polisi, huku hawajafuata taratibu hizo zote wala hawajakupa kitambulisho chochote cha kuthibitisha kuwa hao waliojiita ni polisi, kweli ni Polisi.

2. Wananchi ambao tupo karibu, ikitokea watu tusiowajua wanamchukua mwananchi mwenzetu kwa nguvu, kwa kusema tu wao ni polisi, huku hakuna uhakika wowote, na wala hawajafuata taratibu ambazo polisi hutumulia kumkamata mtuhumiwa, moja kwa moja tujue kuwa hao watu ndio maharamia yenyewe yenye lengo la kumpoteza mwananchi mwenzetu. Hivyo ni muhimu kuchukua hatua za haraka ili kumwokoa mwenzetu. Kwa kuwa haya majitu ni maharamia yanayowamaliza watanzania na kulipaka matope jeshi la polisi, kwa umoja wetu tuyaangamize yote hapo hapo, yenyewe binafsi, na kila kitu yalichokuja nacho, iwe ni gari au kitu chochote yanayotumia kwenye ubaramia wao. Hapa ndipo pa kuonesha ile hasira inayoitwa, "Wananchi wenye hasira kali" Tukifanya hivyo tutakuwa tumelisaidia jeshi la polisi, tumeokoa maisha ya mwenzetu, tumelinda maisha ya wengine ambao walikuwa njiani kutekwa, na pia tutakuwa tumeisaidia Serikali, maana hatimaye tutajua hayo maharamia yanatoka wapi, yanatumwa na nani, na yanafanya hayo kwa lengo gani.

NB: Viongozi wa dini kwa kuwa mnakutana na wananchi wengi kwa pamoja na kwa kila wiki, ni muda sahihi sasa wa kuwapa waumini wenu tahadhari ya hii hatari ya utekaji, na kuwaongoza waumini wenu namna ya kusaidiana pale inapotokea mwenzao anaonekana yupo hatarini kutekwa.

HATUA YA AWALI:
Kila mwananchi atembee na filimbi. Ukiwa kwenye hatari ya kutekwa au ukaona mwenzako anafanyiwa vitendo vinavyoashiria ni utekaji, puliza filimbi mara moja, na wote tuliosikia filimbi, twende kwenye tukio kumwokoa mwenzetu na kila aina ya silaha itakayosaidia kumwokoa mwenzetu..

Huu ni wakati wa kujitetea na kushiriki katika ulinzi wetu binafsi kuliko kuwaachia polisi pekee yao.
 
Halafu speaker wa bunge alivyokuwa akizungumza kimasihara leo kuhusiana na hii issue. Sikuweza kutizama tena nikabadili channel fasta.
 
Je wakija na zile 4R na kukuambia ujisalimishe?!
 
Inasikitisha sana!Hivi wananchi wenye hasira kali bado wapo nchi hii?
 
Mungu atusaidie! Kwa sasa watanzania tunatawaliwa kimafia.
 
Back
Top Bottom