Kupambana na watu wasiojulikana: Ukija kukamatwa na polisi bila uniform na hajaambatana na kiongozi wa eneo husika piga firimbi, kusanya nzi

Kupambana na watu wasiojulikana: Ukija kukamatwa na polisi bila uniform na hajaambatana na kiongozi wa eneo husika piga firimbi, kusanya nzi

Siyo kweli kuwa maaskali wote ni waajiriwa wa CCM,huwa ni stress za maisha ndo zinawasumbua dhidi ya hii Serikali dhalimu hivo mtu yeyote akikatiza mbele yao najua jibu unalo.

Huwezi leta utani mbele ya mtu mwenye hasira.

Fikiria asikari polisi yeyote yule ambaye hana nyota anafanya hiyo kazi kama kibarua kwa miaka 12 bila kuwekewa pesheni kama walivyo wafanyakazi wengine.

Ndo tatzo linalowatesa hawa ndgu zetu, tuwaomee huruma.

Na ukifungua mdomo kwa hili jambo adhabu Kali sana zitakuandama na hata kukosa promotion zingine.
TUWAOMBEE
 
Siyo kweli kuwa maaskali wote ni waajiriwa wa CCM,huwa ni stress za maisha ndo zinawasumbua dhidi ya hii Serikali dhalimu hivo mtu yeyote akikatiza mbele yao najua jibu unalo.
Huwezi leta utani mbele ya mtu mwenye hasira.
Fikiria asikari polisi yeyote yule ambaye hana nyota anafanya hiyo kazi kama kibarua kwa miaka 12 bila kuwekewa pesheni kama walivyo wafanyakazi wengine.
Ndo tatzo linalowatesa hawa ndgu zetu,tuwaomee huruma.
Na ukifungua mdomo kwa hili jambo adhabu Kali sana zitakuandama na hata kukosa promotion zingine.
TUWAOMBEE
Aimen 🙏
 
dah!
kumbe siku zote mlikua hamjilindi?
miljisahau au Imani ilikua kwa Mungu,

lakini sasa mnaamini ushirikina tu na kudanganyana namna za kijadi kujilinda, right? that is very wrong...

umaskini wa fikra na imani potofu ni utumwa mzito sana wa kifukara..

sikilizeni niwasanue, kwanza Muamini Mungu,

lakini pia,
vyombo vya ulinzi na usalama, muhalifu uwe na mawasiliano ama hauna, umejilinda ama vinginevyo. ukiwa muhalifu utatafutwa popote ulipo, utatiwa nguvuni na kisu au silaha za kijadi ulizonazo, na utawajibika kwa uhalifu wako mujibu wa sheria bila mbambamba yoyote, msidanganyane 🐒

Malaika Mkuu Gabriel atuondolee unyonge na hofu zisizo na maana yoyote na atulinde na adui muovu sote, sasa na hata milele .
Amina
Samahan kukwambia iko miamba enzi zangu nikiwa service, ilipotea kwa hewa na haijawahi kukamatika mpaka leo. Si wote wanakamatwa kuna manguli
Japo hao wako wachache sana
 
Njia nyingine kwa mtu anayehisi anawindwa na hao wahuni, ni kuhakikisha anakula vyakula ambavyo vinaweza kutengeneza bomu la nyuklia ndani ya tumbo!

Yaani kila siku ahakikishe vyakula kama maharage, mayai ya kuchemsha, mahindi ya kuchemsha, mtindi, nk. Halafu hao wahuni wakimteka, akubali tu kuingia kwenye gari lao. Gari likiondoka tu, alipue sasa hilo bomu 💨 halafu aone watakavyo poteana!
 
Njia nyingine kwa mtu anayehisi anawindwa na hao wahuni, ni kuhakikisha anakula vyakula ambavyo vinaweza kutengeneza bomu la nyuklia ndani ya tumbo!

Yaani kila siku ahakikishe vyakula kama maharage, mayai ya kuchemsha, mahindi ya kuchemsha, mtindi, nk. Halafu hao wahuni wakimteka, akubali tu kuingia kwenye gari lao. Gari likiondoka tu, alipue sasa hilo bomu 💨 halafu aone watakavyo poteana!
Swadakta
 
Sahivi kila mmiliki smartphone anasema kuna cruiser inamfatilia kwa nyuma
 
Samahan kukwambia iko miamba enzi zangu nikiwa service, ilipotea kwa hewa na haijawahi kukamatika mpaka leo. Si wote wanakamatwa kuna manguli
Japo hao wako wachache sana
nakubali nguli 👊💪
 
Kuna watu kukamatwa wanajitakia,mtu unajua unatafutwa halafu unalala nyumba ile ile ya kila siku lazima udakwe.Ukijua unatafutwa badilisha nyumba ya kulala,mtaaa hadi sehemu usilale sehemu 1 zaidi ya siku 1.
 
Dawa ni kuweka kidumu cha petrol home,Wakija watu usiku na gari bila plate number halieleweki,mwagia wese tia kiberiti
 
Wakuu kwema,

Watu wasiyojulikana siyo maneno mageni kwetu, na mambo haya yameanza kitambo kuanzia enzi za Kikwete na Ulimboka (kusoma tukio hilo zaidi hasa kwa Gen Z soma hapa - Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sanaaliyetekwa na watu wasiyojulikana na kukukwa ametupwa kwenye msitu akiwa ameteswa sana na kung'olewa meno.


Kadri awamu zilivyobadilika na ndivyo matukio haya yamezidi kuongezeka, na sasa wamekuja na mbinu mpya.

Wanakuja watu wanaojitambulisha kama polisi na kutaka kukukamata, lakini wanakuwa wamevalia kiraia yaani hawana gwanda za polisi, watakuonesha kitambulisho (lakini hivi hata vya mchongo vinapatikana), wakiwa pia na gari binafsi, nyingi ambazo zimekuwa zikihusika ni Noa nyeupe au nyeusi, au zile Cruza, lakini pia jamaa huibuka wenyewe wenyewe tu bila kiongozi wa husika.

Kuelewa zaidi haki yako pale polisi anapokuja kukukamata soma: Jua haki yako unapokamatwa na Polisi

Mfano wanakuja mtaani kwako lakini mjumbe wa eneo husika hana taarifa, au anafika sokoni lakini hawaambatani na uongozi wa soko.

Polisi wakishutumiwa kuhusika na matukio haya wanakana, kwamba waliofanya matukio hayo siyo polisi, wanauliza uongozi wa eneo hilo ulikuwepo? Walikuwa na uniform? Walitoa vitambulisho? Walikuja na gari ya polisi?

Ukiangalia ni kweli sababu hawaendi na utambulisho wowote kuwa wale ni polisi, ni tobo (loophole) tunalotakiwa kuliziba, huku polisi wakitoa matamko polisi akija kwa namna hiyo (bila utambulisho official) basi mtuhumiwa anatakiwa kukataa kukamatwa!

Pia soma: Sativa225 (Edgar Mwakabela) kijana maarufu kwa kukosoa serikali X apatikana, baada ya kutekwa na watu wasiojulikana

Hapa kwenye kukataa kukamatwa ndio kunaleta ka ugumu, maana tuambiane ukweli kuwadindishia wajeda labda na wewe mwenyewe uwe na msuli, vinginevyo unapigwa makofi mawili, unashikwa kwenye pindo ya suruali huyo ndio umeenda hivyo.

TUFANYAJE SASA KUKABILIANA NA HAWA JAMAA WANAOITWA WATU WASIYOJULIKANA?

Bila wananchi kushirikiana hatuwezi kushinda hili, inabidi tuwe na umoja kama tunavyoshadadia mambo ya kijinga.

Kwenye maandamano yanayoendelea Kenya ili mwandamaji aepuke kukamatwa ovyo walikuwa wanatembea na firimbi, akiona ameshindwa anaichomoa fastaa anaipuliza wenzake wanajaa kuhoji kuna nini, tuitumie njia njia hii.

~ Ukiona watu wanaojitambulisha kama polisi hawajavaa uniform zao, wana gari private na wakati mwingine hakuna plate number, na wala hawajaambatana na uongozi wa mtaa/eneo husika wanang'ang'ana kukuchukua usiende kizembe, puliza firimbi yako, puliza kwa nguvu zako zote kushutua watu wajae.

- Huna filimbi siyo kesi, piga kelele, yaani PIGA KELELE kwa nguvu zako zote mpaka watu wajae, hapa na wewe usiwe mzembe, sema hawa wanadai ni polisi lakini hawana uthibitisho kuwa wao ni polisi.

- Tutumie simu zetu vizuri, wakati jamaa aliyeshikwa anapayuka na kelele zake, wengine rekodini kila kitu, tupate sura zao, pamoja na usafiri waliokuja nao. Namba halisi ya gari huwa inaandikwa kwenye kioo cha gari pale mbele upande wa dereva kama sijakosea, maana kuna uwezekano mkubwa plate iliyotumika ni fake chukueni video na ya namba hizo. Wengine mko vizuri kwenye utaalamu wa mitandao ya kijamii, badala ya kurekodi kwenye simu yako ingia kwenye mtandao wowote wa kijamii na urushe tukio hilo live, amini nakwambia ni dk 0 tu litakuwa limeshasambaa nchi nzima na hao jamaa hawatochomoka.

- Wakati hayo yanaendelea wahojini watu hao ni kina nani na wanatoka wapi, kwa kiasi kikubwa ili kuua soo wataingia kwenye gari na kusepa ili wasitambulike zaidi, ikiwa watatoa silaha, ni muhimu kujilinda, wakifanikiwa kuondoka na jamaa walau tutakuwa na utambulisho wao wote kuanzia sura mpaka namba kamili za usajili.

Kufanya hivi itakuwa rahisi kuwatambua watu hawa wanaotekeleza matukio hayo, na tukiwabaini ni polisi, Jeshi la Polisi litatueleza vizuri kwanini wanashiriki kwenye mauaji ya raia.

Kama nilichokiweka kina manufaa sambaza ujumbe kwa ndugu na jamaa tushirikiane kukomesha watu hawa wasiyojulikana.
Naunga mkono hoja hakuna aliye salama
 
Hiyo mbinu yako inaweza kufanya kazi endapo tu watakuja mchana kweupe au hata usiku ktk halaiki ya watu lakini mazingira tofauti na hayo ni ngumu hata kupiga yowe/filimbi.

Wakija nyumbani kwako either kwa kuvunja mlango au kwa kubisha hodi au wakikuta sehemu tulivu huku wamekushikia mtutu wa bunduki hautakua na hiyo nguvu ya kupiga yowe, zaidi watakuambia ingia ndani ya gari kabla hatujakumwaga mavi muda huo huna nguvu ya kowahoji hapo ni kutii amri yao tu.

Labda utupe mbinu wakikukuta upo nyumbani pekeyako au na mumewako/mkewako na watoto kipi cha kufanya.
kutii ami ni kukitii kifo ambacho ukitii utakufa usipotii utakufa sas bora ufe ukipambana kujiokoa mait inaez bak ikazikwa ht na ndugu zko kuliko kua kondoo ukazkwe na site au ukaliwe na wanyama
 
Siku viongozi wa dini wakiona hili ni tatizo kubwa na wakajitokeza kwa pamoja (mfano Baraza la Maaskofu Tanzania) wakaitisha press kwa pamoja na wanakasema hili ni tatizo, au baraza la maulamaa wakasimama kwa pamoja nchi nzima wakaitisha press wakasema hili ni tatizo, pamoja na wale wengine wa katika umoja wao, Mambo haya yataleta matokeo chanya sana kwenye jambo hili.
Ninachokiona mm kwa sasa, viongozi wa dini wameamua kuendelea na shughuli zao tu, Mambo haya wanayasemea kwa asilimia moja kati ya mia kwenye mikusanyiko yao.
Hawana haja ya kukutana na Serikali faragha, watoe utaratibu na wawahimize waumini wao kujitetea.
 
Back
Top Bottom