Kupanda kwa bando kuathiri kilimo na ufugaji. Video call zilipunguza sana udanganyifu. TCRA msilichukulie poa

Kupanda kwa bando kuathiri kilimo na ufugaji. Video call zilipunguza sana udanganyifu. TCRA msilichukulie poa

mgt software

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Posts
13,778
Reaction score
7,145
Wana Jf.

Wakati serikali ikijitahidi sana kuingiza fedha nyingi kwenye kilimo, makampuni ya simu yapo mstari wa mbele kuumiza matumiaji wa Internet kwa kuongeza gharama lukuki kila mwezi. Uwezi kumaliza mwezi kabla ya vodacom na airtel hazijapunguza vifurushi vya bando. Hii ni kudidimiza juhudi za Mama ambazo amewekeza katika kilimo.

Hiko hivi. Kwa kuwa wakulima wengi hawana mitaji, kuna baadhi ya wafanyakazi wengi wenye mitaji wameingiza fedha nyingi katika kilimo, uwekezaji huu umetumiwa na watu wengi sana kuongeza uzalishaji na mnyororo wa thamani. Unakuta mfanyakazi anapokuwa likizo nyumbani anaseti miradi, anaweka wafanyakazi alaf anawafuatilia kwa simu. Nyakati nyingi watu wa aiana hii wananunua simu zenye uwezo mkubwà wa kuona kwenye kamera, anaweza kuzuru shamba lake kwa kutumia video call. Hii ilikuwa inaondoa usumbufu wa gharama za kukagua shamba lakini pia kujua undani wa mtu uliyemwajiri kama anawajibika ipasavyo.

Ukaguzi katika kukagua kitu unachonunua wengi wanatumia video call na voice call kubagain na kutumiwa kitu ulichochagua. Sasa kuongezeka kwa bando ni mzigo mwingine. Tuliaminishwa kuwa tukiwa na mkongo wa taifa Internet itakuwa ya gharama nafuu zaidi. Wajenzi wa mikonga tuliwaona kila mkoa mpaka zoezi likakamilika. Sasa inakuwaje bando linakuwa ghali zaidi? Au mawaziri wasio waaminifu wanashirikiana na watu wa mawasiliano kutupiga kwa kuwa wanaona matumizi ya Internet yameshika kasi? NAPE kila siku anawatetea, sijui hajui kuwa habari ya kusimikwa kwa mkongo tunayo? Au anatufanya hatujui lolote wakati wakulima wa sasa pia ni wafanyakazi.

Nape utamwangusha Mama ikiwa umepewa wizara nyepesi kushinda ya Makamba bado unasimamia ukandamizaji. Mwaka jana mwezi wa 2 bando la 1000 ulikuwa unapata dakika 60, 1Gb na sms 3000 leo hii 1000 unapata 450mb na 30dkk , hivi kumetokea nini? Mmetupiga kwenye kunuanua tunachangia tozo bado hamurìthiki?
 
Sema baba sema, hatuoni kabisa faida ya huu mkongo.
 
Back
Top Bottom