Kupanda kwa bei ya mafuta kumevuruga biashara yetu ya mbogamboga

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Kijana wangu alitafuta ajira kwa miezi sita baada ya kumaliza chuo. Mwisho tuliamua kuingia katika kilimo cha mboga mboga.

Shamba ni la urithi la ekari tatu, tulikodi trekta kung’oa visiki. Tulichimba kisima na kununua simtank la litre 3,000 pamoja na pump yake. Ilibidi kujenga kibanda na kuajiri mtu kwa mshahara wa laki moja na nusu. Huyu alimwagilia bustani na kuchuma mboga alfajiri.

Ilibidi kupata mkopo wa kununua pick up double cabin used. Alfajiri kijana alipeleka sokoni bamia, nyanya, mchicha na hoho. Kwa siku alipata laki 350/400. Hapa kuna gharama za mafuta, na kuweka marejesho ya mkopo wa gari.

Sasa hivi baada ya kupanda kwa gharama za mafuta, mpaka kufikisha mboga sokoni ni karibu laki na nusu kwa mafuta tu. Licha ya hivyo wanunuzi hakuna na mboga zinarudi.

Hasara imekuwa kubwa hata mshahara wa mfanyakazi wa shamba imekuwa vigumu kuupata.
 
Pole mkuu, hizo ndio changamoto, punguza route ongeza muda wa kukaa sokoni.
 
Uza hilo shamba upate pesa,
Ukipata pesa utaitwa pedeshee,
Utatembelea sehemu za starehe ule maisha.
Ukijibana bana utakufa kwa presha na maisha ni mafupi.
Chukua ushauri huu na utakuja kunishukuru.
Pichani ni ndugu Mwai kibaki akipigiwa saluti akiwa amelala mavumbini
 
Rais anazikwa kama ng'ombe?[emoji15][emoji15]
 
Mimi ni mkulima pia mambo yamekuwa magumu upande wa umwagiliaji hasa bustani na zinataka maji kwa kiasi kikubwa!!

Ila hapa kama kuna mtu pia anaweza kutufungua akili atueleze hivi hakuna water pump zinazotumia nguvu ya jua?

Nimejaribu kutumia zile money maker pump kukanyaga kwa miguu ila mashamba ni makubwa asee ! Na mtu anachoka sana!
 
Zipo solar water pump, pesa yako tu bwashee


#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana aisee, kwa hivyo mbogamboga watu wameacha kula baada ya mafuta kupanda, na sasa wamehamia kwenye ulaji wa nyama nyeupe kuku, Bata na samaki
 

Zipo za upepo, windmill.. inavuta maji na inazalisha umeme at the same time.. sema sio chini ya M5
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…