Kupandisha bei ya sabuni kutampa maskini muda mgumu katika maisha

Kupandisha bei ya sabuni kutampa maskini muda mgumu katika maisha

Mung Chris

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2017
Posts
3,474
Reaction score
4,007
Leo nimeenda kununua sabuni ya mche ya Jamaa, bei niliyoijua ni sh 2,000 kwa mche, kuanzia leo baadhi kila nilipofika nikajua nitapata kwa bei ya zamani nimeambiwa imepanda wanauza 2,200 hadi 2,400.

kati ya bidhaa ambazo wasio na uwezo huhitaji haswa ni Sabuni, Sukari, mafuta... vyote hivi vimekuwa vikipanda kiasi kwamba itafikia hatua wasio na uwezo hawata tumia kabisa watatafuta mbadala.

Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha bidhaa watumiavyo maskini havipandi ili kuathiri mfumo wao wa maisha ukizingatia kuwa kipato chao ni kidogo sana.
 
Bado minne mkuu!! Vuta subra..ama kama vip!!!.

MITANO TENA:
 
Hii ni hatari sana
Kabisa mkuu bado hata kati hatujafika

Ngano kilo 1500 toka 1100

Bado mi4 🍺
huu ndio uchumi wa kati unao tupeleke kwenye ongezeko la bei za bidhaa watumiazo maskini?
 
Kati ya Nchi ambayo haijali matumizi ya bidhaa za nyumbani kwa bei zake zisizoeleweka Tanzania ipo mafuta hayajawahi kuwa dili eti sasa hivi nayo dili sukari wamejiwekea pin code ya kupiga Kodi huko basi kila kukicha inapanda bei Nchi majirani ambao ni wazalishaji wakubwa bei ni nusu ya Tanzania kwa kilo faida ya kuwepo viwanda nini sasa kama bei za bidhaa za hapo hapo zipo juu...
 
Sio Mitano tena ni milele kabisa...
Uchumi wa kati....
Nchi hii ni tajiri sana...
Au nasema uongo ndugu zanguuuuu...
Unaijua vieite wewe!!!
Sisi tunatembelea mavieitee!!!
 

Attachments

  • IMG_20210127_125033.jpg
    IMG_20210127_125033.jpg
    86 KB · Views: 10
tulikubaliana mwisho kupandisha bei kwenye mafuta ya kula, na sabuni tena?
 
Back
Top Bottom