Kwanini unafanya kazi na kwanini kazi fulani na sio kazi nyingine ?
Je kazi ni means to an end au unafanya kazi fulani sababu upo enganged kwenye hio kazi hivyo basi bila hata ujira ungeweza / ungependa kuifanya
Majibu yako hapo yanaweza kukwambia kama jamii tumekuwa na utamaduni wa kuweka a Cart before a Horse..., Hivyo usishangae mtu ni Bwana Shamba na analalamika kupangiwa kazi sehemu zenye wakulima na mashamba,
By the way huenda hata baadhi ya vijiji vya leo yana facility kuliko hata miji ya zamani; kama ni habari na connectivity ya dunia yote kinganjani hivyo kuweza kujiendeleza ni uamuzi tu.....
Baada ya kuona baadhi ya watu wanadharau shule na wengine kuona kwamba shule ndio kila kitu hadi kujipachika Sifa za Kuelimika nimeona tukumbushane Qoute ya Mark Twain; (Writer, Humorist, Enterpreneur, Lecturer) na School Drop- Out Don't Let Schooling interfere with your Education....... Ni...
Yaani wife wamemtupa huko porini... hapa nawaza ikipita mwaka niweka dau la 5 milllion apatikane mwalimu wa kubadilishana naye... ikishindikina sijui itakuwaje
Kupangiwa kazi vijijini kunapoteza ndoto za wengi katika hali tofauti tofauti
Masista duu wengi hasa walimu waliokuwa wanawaza kuolewa na washikaji zao wa Dar wenye vibunda, kila wakihangaikia uhamisho serikali inabana umri unaenda wameishia kuolewa na walimu wenzao au wakulima wa vijijini.
Chief hivi nikiweka 5 million siwez fanikisha uhamisho wa wife.. ndo kwanza amepangiwa huko kijijini.. ila nataka nitumie nguvu ya pesa nimrudishe nilipo.. japo sio jijiji ila kwenye halmashauri ya mji
Eee nshawahi kuwa mwalimu bana sisee hapakuwa mbali na mjini ila vimbi kha!
Ukisikia mtu ni mwalimu mpe heshima zake mimi yalinishinda.
Sijui mnanielewa ama? Ati wanafunzi wakifunga mimi nibaki maeneo ya shule yaani siwezi kwenda nyumbani kama sina likizo ati nibaki nareport shulen kila siku 🤣
Kubwa kuliko yote nikibaki shulen kumbuka wanafunzi wako likizo shulen nakutana na mbuzi ndo zinakuwa zinazunguka viwanjani nyieeee!
Kuandaa sijui assessment sijui ya mwaka sijui nini dah!
Kunifanyia eti kukaguzi wa kustukiza tena niko darasani, siku hiyo nilimuacha darasani nikawaaga wanafunzi nikawaambia sijiskii vizuri.
Bado kufika kazini ikishafika saa 7:30 kitabu cha kusaini kusharudishwa kwa HM
Vumbi la barabarani nikiwa naenda kazini nyieeee!
Wachawi kulala wananiniga usiku!
Niliandika barua ya kwenda masomoni na ndo ukawa mwisho wa ualimu.
Nyie heshimuni watumishi walioko vijiji hasa walimu dah.
Ikawaje mkuu... ? Uliacha utumishi wa umma au ilikuwaje? Maama mimi wife na yeye kapata ualimu ... ni wa msingi sasa nawaza sana hapa sijui nifanyeje... nataka kutumia nguvu ya pesa sijui kama itawezekana
Kama ni mjasiliamali pesa hazikosi kazi,unajenga zizi la kukusanyia wanyama toka kwa wanakijiji mmoja mmoja mwenye shida wakifika wa kutosha unawatia kwenye fuso mjini,ukitoka mjini unalijaza bidhaa za jumla unajaza kwenye nyumba yako kijijini unaanza wasambazia viduka vidogo vidogo vya vijijini huku unanua mazao na mifugo huku unalimisha kwa mnyororo huohuo kwa mwaka mzima.
Kijijini kwa asiye na asili ya ujasiliamali apamfai
Kwa nini volunteers kutoka Ukaya na USA wanamudu kuishi vijijini Tanzania bila malalamiko? Msiseme wote ni wapelelezi! Wengine ni raia wa kawaida kabisa na wamekuja Afrika kupata ajira wakitokea huko kwao.
Ni ujinga tuu unakusumbua,Cha maana ulichofanya hapo mjini ni kipi? Kwa kuwa unaunga unga ndio maana uliomba kazi ya chini ya 800k Kwa mwezi.
Sasa wenye akili wanataka wapangiwe Vijijini maana ni fasta unakuwa Tajiri..
Harafu mlivyo mbumbumbu mnadhani Vijiji vya Leo ni sawa na vya zamani,Kwa taarifa yenu Vijijini karibu vyote vina umeme,Barabara na issue ya Maji Ruwasa wako kazini..
Ukiniuliza Mimi Vijiji vigumu labda ni vile ambavyo Kilimo,uvuvi na ufugaji havifanyiki..vyenye Hali ya ukame
Hapa shida ni Serikali kwa kushindwa kutengeneza mazingira rafiki ya mtumishi kufanya kazi kijijini ilibidi watumishi wa vijijini wapate angalau motisha za nyumba bure na kusamehewa loan board na wawe na posho ya kufanya kazi kijijini ili watu wahamasike.
Kinachoumiza watu wa vijijini ni kuona salary yao sawa na wa mjini halafu wao wako porini penye shida ya huduma za kijamamii mtu huyu lazima aombe kuhama ikishindikana ndio unasikia kaacha kazi.
Kwanza safi sana ndio mkome maana wakati Serikali inasema ikate tozo ya miamala na tozo ya mafuta Ili iimarishe Huduma za jamii Vijijini mlikuwa hamtaki mnapiga makelele sana huko Mjini..
Mlidhani mnaikomoa Serikali mkasahau kwamba mtaomba kazi zenu hizo ya ualimu,nursing,udaktari,utendaji wa Vijiji na kata,uafisa ugani ,Polisi na kazi zingine kama hizo..
Ni hivi hutaki kazi tena,uliomba Kwa vile huna jeuri ya kipato na itafanya tuu yaani hizi ni kelele za Sasa hivi ila utakuwa mwanakijiji saaafi kabisa..
Ni kama vile mtu anashabikia wafungwa kufanyishwa kazi za kikatili anasahau kwamba ipo siku unaweza kuwa mfungwa Kwa bahati mbaya au vinginevyo.
Umeuliwa vipi wkt imekaa miaka mitano mtaani hujafanya maajabu yoyote, sema ulikuwa tayari umeshakufa kitaaluma na kifikra, shukuru umepata pa kuanzia tena.
Tanganyika ni Wilaya nzuri Kwa kilimo na inafikika vizuri,Tarura imefungua mawasiliano kufika kusiko fikika ,pia umeme upo karibu Vijiji vyote Kwa Sasa.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.