Kupangiwa kazi vijijini tayari unakuwa umeuliwa kifikra na kitaaluma

Kupangiwa kazi vijijini tayari unakuwa umeuliwa kifikra na kitaaluma

Motivesheni supika
Kama ina-serve the Purpose na ku-wamotivate watu sioni tatizo lolote, ubaya ni kuwapa watu false hopes na kuwadanganya ila narudia nilichosema tangia mwanzo issue ni wewe na sio wao unataka nini (hizo ndio fikra za kukujenga wewe binafsi) ukishajua unachohijati utawekeza nguvu kuelekea huko, Kama haujui unataka nini utakuwa una-chase an illusion ambayo haina mwisho - unaishi maisha fulani ya mashindano ambayo hata unaoshindana nao hawajui kwamba una-exist.....; Kwahio sikupangii kama hutaki kuishi kijijini usifanye hivyo na kuendelea kwako kuwa hapo haujitendei haki...., ila kama wewe ni Bwana Shamba na haupendi kuishi kijijini you made a wrong career choice from the get go....., Kama wewe ni mwalimu motivation yako kubwa ni kufundisha na kuelewesha watu, hivyo kama wanaohitaji elimu wengi ni vijijini nadhani hio ni purpose tosha ya kukufanya wewe uende huko na uki-dig deep huenda ukafanya uchunguzi na kuja na njia mbadala na majibu kwanini huko wengi wa watu wanahitaji elimu.

That said huenda wanahitajika motivational people wa-kuwamotive watu waelewe kwamba maisha ni pale ambapo panakufaa wewe..., na katika kazi jaribu kufanya kazi unayoipenda sababu hayo ndio maisha yako; ukizingatia shughuli hizi za kubangaiza maisha yako asilimia kubwa unaitumia either ukiwa umelala au kazini.....
 
Ni ujinga tuu unakusumbua,Cha maana ulichofanya hapo mjini ni kipi? Kwa kuwa unaunga unga ndio maana uliomba kazi ya chini ya 800k Kwa mwezi.

Sasa wenye akili wanataka wapangiwe Vijijini maana ni fasta unakuwa Tajiri..

Harafu mlivyo mbumbumbu mnadhani Vijiji vya Leo ni sawa na vya zamani,Kwa taarifa yenu Vijijini karibu vyote vina umeme,Barabara na issue ya Maji Ruwasa wako kazini..

Ukiniuliza Mimi Vijiji vigumu labda ni vile ambavyo Kilimo,uvuvi na ufugaji havifanyiki..vyenye Hali ya ukame
Asante MWEREVU.

#YNWA
 
Kuhama inawezekana ila sio rahisi kiasi hicho.

#YNWA
Juinge CCM,gombea Uongozi uchaguzi wa 2027,ukishinda hasa zile nafasi za ngazi ya wilaya,mkoa au Taifa kuhama ni chapu

Maana tayari utakuwa ushatengeneza koneksheni na wakubwa,kwani ukipata Uongozi wa ngazi ya wilaya,mkoa aua Taifa tayari ushakuwa kwenye circle ya ma DEO,DED,DC,RC na wengineo

Jiongeze

Miye nipo Tanganyika,kwetu Iramba,chaki nakula na Bata nakula

Nalima,nafuga,natengeneza kucha na pia nipo ndani ya CCM hivyo kumi kumi na laki laki za vikao wilayani,Mkoani au Taifa hazinipiti mbali
 
98% ya wafanyakazi wote wa huku wanataka kuhama.

98% ya wafanyakazi wote wenyeji wa huku waliopangwa maeneo mengine hawataki kurudi huku kwa Uhamisho wa kubadilishana.

98% ya wenyeji wa huku wamekimbia maeneo mengine, huku wanarudi mwisho wa mwaka.

Hiyo ndio hali halisi.

Nyingine porojo tu na ubishi wa ajabu ajabu
Niliamua kuacha kuendelea sababu niliona najirudia kama rekodi mbovu, uli umeniqoute pengine ngoja nikujibu na hapa

Aliyesema watu wanapenda kufanya kazi huko au panafaa kwa watu kufanya kazi ni nani ? Rudia kusoma ulichoandika na nilichokujibu; kuna sehemu umeandika huko huwezi hata kufuga kuku sababu chakula ni cha kununua na palepale umeongelea kwamba ukisema utengeneze chakula kila mtu anafanya (automatically hapo kuna supply na demand) Kwahio kama haipo issue kubwa ni utamaduni wa hapo na ugumu wa mgeni kupewa ushirikiano; Uwepo wa Tatizo na Sababu ya Tatizo lililopo sio lile ulilosema wewe...., Narudia tena rudia kusoma ulichoandika na nilichokujibu sababu nahisi na hapa utakuja na majibu mengine ambayo huenda mjadala utazidi kurefuka kwa kuongezea vipengele ambavyo vitarefusha mjadala to infinity.....

Kumbuka hapa ni kuuliwa kifikra na kitaaluma sasa kama taaluma yako ni mwalimu huoni hii ni food for thought ya kujiuliza kwanini watu wa kada lenu wengi inakuwa ngumu ku-assimilate huko na ni nini kifanyike au kijaribu kufanyika (When in Rome; Do as Romans....)
 
Yaani wife wamemtupa huko porini... hapa nawaza ikipita mwaka niweka dau la 5 milllion apatikane mwalimu wa kubadilishana naye... ikishindikina sijui itakuwaje
Lazima umegewe na Afisa Elimu,Mwalimu Mkuu/Mkuu wa shule ,DED nk 🤣🤣🤣🤣

Unaweza pata uhamisho.kama. una Ndoa lakini ni uhamisho wa kumsogeza sehemu inayofikika kirahisi Kwa sababu ataambiwa tuu mjini nafasi hakuna ila ipo jirani na mjini chagua na hongo utatoa.
 
Bro Uzi wako nimeuona na nimeulewa sidhani Kama Kuna halmashaur iliibuka tu na kuwa na huduma zote za kijamii
Ni uongo bro kwa mfano mzuri mm Niko halmashaur ya momba Ni WILAYA changa na mpya
So naamini one day tutafikiwa Ni wilaya inayokuja kwa kasi sana
Alfu pia nikutoe mawazo yako chanya eti ukiwa kijijin akili inalala
Ukipangiwa kijijin huwezi pata nafasi ya kwenda kusoma Ni uongo
Hapa kituoni nilipo Kuna mtumishi mwenzangu kapata nafasi kaenda shule
Kikubwa kushukuru mungu tu now days AJIRA NI NGUMU UKIPATA SHUKURU
hayo mengine utajua mbele ya safari
 
Inabidi fikra zetu tujiulize yafuatayo :-
  • Kwanini unafanya kazi na kwanini kazi fulani na sio kazi nyingine ?
  • Je kazi ni means to an end au unafanya kazi fulani sababu upo enganged kwenye hio kazi hivyo basi bila hata ujira ungeweza / ungependa kuifanya
Majibu yako hapo yanaweza kukwambia kama jamii tumekuwa na utamaduni wa kuweka a Cart before a Horse..., Hivyo usishangae mtu ni Bwana Shamba na analalamika kupangiwa kazi sehemu zenye wakulima na mashamba,

By the way huenda hata baadhi ya vijiji vya leo yana facility kuliko hata miji ya zamani; kama ni habari na connectivity ya dunia yote kinganjani hivyo kuweza kujiendeleza ni uamuzi tu.....

Asilimia 90 ya mabwana shamba/Mifugo wanaishi Mijini Sasa mwaka ujao wa Fedha Serikali imesema inaenda kujenga nyumba 4,000 Ili wajae huko huko kwenye kata zao na kumbuka wanariooti Kwa Mtendaji Kata so hatua Kwa hatua wowote wataishi Vijijini
 
Back
Top Bottom