Kupangiwa kazi vijijini tayari unakuwa umeuliwa kifikra na kitaaluma

Kupangiwa kazi vijijini tayari unakuwa umeuliwa kifikra na kitaaluma

Acha aka report mkuu walau mwaka kupata barua ya uthubitisho Cheti Cha ndoa Kiko???????? Unaweza piganisha unaumwa unahitaji support yake now huduma inafanyika online
Asante sana mkuu, bahati mbaya cheti cha ndoa sina... itabidi ndani ya huu mwaka nikipate harakati zikifika mambo yawe straight forward
 
Lazima umegewe na Afisa Elimu,Mwalimu Mkuu/Mkuu wa shule ,DED nk 🤣🤣🤣🤣

Unaweza pata uhamisho.kama. una Ndoa lakini ni uhamisho wa kumsogeza sehemu inayofikika kirahisi Kwa sababu ataambiwa tuu mjini nafasi hakuna ila ipo jirani na mjini chagua na hongo utatoa.
Akimegwa atajua mwenyewe... K si yake bhana... mbaya ni kujua tu mkuuu...

Anyway, kitajulikana tu ngoja mwaka upite
 
Ulishawahi kufika kijijini wewe?
Nilizaliwa kijijini, nimesoma primary kijijini, sekondari na chuo ndio nilisoma mjini.

Ajira ya kwanza nilifanya na Swedish Salvation Army, Dar_es_Salaam. Ajira ya pili nilifanya na Benki ya Damu kwa ufadhili wa CDC, ilikua Njombe (wakati huo bado Iringa), baadae nikaingia serikalini nikapangiwa wilayani, baada ya kuridhika na utendaji wangu wakanikabidhi kituo peripheral, kijijini hasa, mpakani.
 
Purchasing power ya watu wa kijijini ni ndogo sana.wananchi wamechoka hawana hela utawauzia nini wanunue? Hta hayo maziwa utamuuzia nani ikiwa kila mji una ng'ombe zake.
Miuu kukaa kijijini hakuzuii kufata soko mjini, kwa mfano mimi nilikua natoa mbuzi Malawi, wanafika kijijini, ninanenepesha na wengine walikua wanazaa, na nilikua nikiwauzia wilayani.

Lakini pia niliwahi kutoa bidhaa kijijini wilayani Kyela, na kuuza Ilembula na Makambako.
 
Ajira Mpya msitishwe Kuhusu Vijijini na watu wa Mjini , Vijijini Kwa Sasa Kila kitu uhakika kuanzia umeme Hadi Maji
 
Kijijini fursa nyingi sana, hasa kwenye sekta ya ardhi, kilimo, ufugaji (ng'ombe wa maziwa, mbuzi...), usafirishaji, uvuvi (kwa baadhi ya maeneo), maji, na viwanda vidogo (kama kufyatua tofali, kutengeneza makochi, kushona nguo...).

Pia kijijini wana jamii wanakuwa na ushirikiano mkubwa sana kwa wataalamu wa afya, jambo linalokupatia faraja kubwa ambayo ina thamani kubwa isiyoweza kupimwa kwa kipato cha pesa.

Kijijini pia unapata muda wa kuwa karibu na familia yako kama unayo.

Kijijini unaweza kupata nyumba ya serikali bure, au ukapata nyumba nzuri kwa gharama nafuu, hivyo kusave something.

In short kijijini fursa ni nyingi kuliko mjini kwa watu wenye mshahara unaolingana, na kwa mwenye akili inachangamka zaidi nje ya your comfort zone kuliko kudumaa mjini na vijiwe (kufanya fani moja pekee).
Mkuu sio rahisi kihivyo huko ndio unaweza Kuta mtu anagawa maziwa Hana kwa kuyapeleka ni rahisi sana kulizungumzia kama hujafika eneo la mradi
 
Mkuu sio rahisi kihivyo huko ndio unaweza Kuta mtu anagawa maziwa Hana kwa kuyapeleka ni rahisi sana kulizungumzia kama hujafika eneo la mradi
Mimi ninakubaliana na wewe, inategemea na kijiji husika, hakuna kukariri, ukifika kijijini ndio unatakiwa kuchangamsha akili.

Hata hivyo ni kweli sio rahisi.

Tumeumizwa sana, ila mwisho wa siku faida ilionekana.
 
Umeuliwa vipi wkt imekaa miaka mitano mtaani hujafanya maajabu yoyote, sema ulikuwa tayari umeshakufa kitaaluma na kifikra, shukuru umepata pa kuanzia tena.
[emoji3581][emoji3581][emoji3581][emoji3581]
 
Katika dunia ya utandawazi kuishi mahali pasipo na umeme wala mtandao kisa kilimo na nyumba za bure zisizo na umeme ni ufala.

Sitakaa eneo la namna hii tena bora kufa masikini.

Wanasiasa wanakula bata kwenye ma-V8 hawakumbuki wenzao wa vijijini eti kisa hata mbuyu ulianza kama mchicha.

Unaweza kuishia kuwa mchicha kiboya
Kama sehemu kuna furusa lakini hakuna umeme bora kuishi sehemu hiyo umeme utanunua mashine
 
Nikipata ajira huko ni mwaka tu au miwili nawabwagia kazi yao.

Serikali inachezea sana hatima za watu
Watanzania mnachekesha sana tangu umetoka chuo uko nyumbani unakula ugali wa shikamoo uwezo wa kubuni kazi huna alafu unazalau kazi heti kijijini kubaya,tangu umetoka chuo umebuni kazi gani?
 
Hivi wewe umewahi Fanya kazi kijijini? Unavifahamu vijiji vya mkoa wa Simiyu au shinyanga? Huku wenyeji hawataki muona mgeni akifanikiwa uchawi Kila Kona tena hadi watumishi wanatumia ndumba hasa wenyeji wa huko unakuta Kijiji kina kaya 400 katika hizi kaya 97 ni za waganga wa kienyeji kaya 250 ni wachawi kaya zilizobaki ndo Zina ahueni umasikini ni WA kutupa halafu kuna mtu anasema vijijini kuna fursa ninawasi wasi utakuwa umetembelea vijiji vya DSM pekee! Kuna vijiji huku greda halijawahi fika kuna Barbara za ng'ombe tu usiombe upate dharula wakati wa masika utajuta.
Buni ajira yako kama uwezi kubali matokeo mfungwa hachagui gereza
 
Kijijini fursa nyingi sana, hasa kwenye sekta ya ardhi, kilimo, ufugaji (ng'ombe wa maziwa, mbuzi...), usafirishaji, uvuvi (kwa baadhi ya maeneo), maji, na viwanda vidogo (kama kufyatua tofali, kutengeneza makochi, kushona nguo...).

Pia kijijini wana jamii wanakuwa na ushirikiano mkubwa sana kwa wataalamu wa afya, jambo linalokupatia faraja kubwa ambayo ina thamani kubwa isiyoweza kupimwa kwa kipato cha pesa.

Kijijini pia unapata muda wa kuwa karibu na familia yako kama unayo.

Kijijini unaweza kupata nyumba ya serikali bure, au ukapata nyumba nzuri kwa gharama nafuu, hivyo kusave something.

In short kijijini fursa ni nyingi kuliko mjini kwa watu wenye mshahara unaolingana, na kwa mwenye akili inachangamka zaidi nje ya your comfort zone kuliko kudumaa mjini na vijiwe (kufanya fani moja pekee).
mkuu kuna watu ni wavivu hata kuwe na fursa gani hawataki kufanya!

imagine mtu yupo kijijini, ardhi ina rutuba, kuna umeme, kuna mitandao ya simu inashika, kuna mazao ya chakula biashara (mchele, viazi, ngano, maharage, mahindi n.k), lakini bado mayai ya kula ananunua, kuku wa kula ananunua, mboga za majani ananunua, mahindi ananunua, maharage ananunua......

alafu analalama kijijini kugumu....... tanzania hii vijiji vigumu kabisa kabisa ni vichache,..... hasa vile vya maeneo ya nusu jangwa...... kwingine ni uvivu wetu tu
 
Mtumishi aliyeko vijijini huko kujiendeleza labda kulima na kufuga huko ila kwenye mambo ya kitaaluma inakuwa ndio mwisho wako.

Huwezi hata kujiendeleza kitaaluma kupitia evening classes maana hakuna vyuo, colleges wala VETA, vyote hivyo asilimia kubwa vipo vijijini.

Kupata ruhusa kwenda kusoma ni kwa mizengwe mingi maana unakuta watumishi wapo wachache.

Wale madaktari wanaotegemea vijiwe baada ya kazi, ukiwa vijijini kwishaaa.

Wewe ndio Daktari pekee zahanati ya kijijini huko, nani atakupa ruhusa ukasome?

NB: Mjini patabaki kuwa mjini tu.
Kijijini changamoto nyingine kubwa ni ulozi
 
Kijijini fursa nyingi sana, hasa kwenye sekta ya ardhi, kilimo, ufugaji (ng'ombe wa maziwa, mbuzi...), usafirishaji, uvuvi (kwa baadhi ya maeneo), maji, na viwanda vidogo (kama kufyatua tofali, kutengeneza makochi, kushona nguo...).

Pia kijijini wana jamii wanakuwa na ushirikiano mkubwa sana kwa wataalamu wa afya, jambo linalokupatia faraja kubwa ambayo ina thamani kubwa isiyoweza kupimwa kwa kipato cha pesa.

Kijijini pia unapata muda wa kuwa karibu na familia yako kama unayo.

Kijijini unaweza kupata nyumba ya serikali bure, au ukapata nyumba nzuri kwa gharama nafuu, hivyo kusave something.

In short kijijini fursa ni nyingi kuliko mjini kwa watu wenye mshahara unaolingana, na kwa mwenye akili inachangamka zaidi nje ya your comfort zone kuliko kudumaa mjini na vijiwe (kufanya fani moja pekee).
Wewe mwenyewe huelewi ulichoandika
 
Back
Top Bottom